Subaru Forester XT vs Kluger

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Wajuvi wa mambo,

Nipeni udambu juu ya hizo gari 2, okoeni ndoa yangu maana shemeji yenu akizimikiwa gari njiani atadai talaka. akikwama topeni ndio kabisa. kwa ufupi wife hapendi vigari sampuri ya ist, impreza nk, anasema anataka gari ya juu juu.

Nimeangalia angalia mitandaoni kulingana na bajeti yangu nimeona hizo akipata mojawapo atanizalia mtoto mwingine.

Nawasilisha.
 
Mkuu, mi sio mtaalamu wa mambo ya ndoa, lakini kwa ushahuri muulize yeye anachotaka, hafu mnunulie ilo ilo analotaka, otherwise utabaki kua na mtoto mmoja forever.

Tuje kwenye magari.

Sijui budget yako, lakini ningekua mimi kati ya hayo mawili ningeenda Klugger IV, ya 2.4L cylinder inline 4. Hiyo ni first gen, ila kama mfuko umenona nenda 2nd gen.

Mbadala wake ningejaribu Harrier 2nd gen.

Mwanamke anahitaji gari low profile. Subaru waachie hao wa mambio.
 
Mkamatie Forester ya kijivu maana nimeona ikiendeshwa na demu inampendeza sana! Kuna mwanamama ana Forester mayai hizi XT namba DWF imekaza sana kila nikimuona natamani hata asimame nimuombe namba ila ndo hivyo yani nashindwa kumfikia.


Kluger nzuri ila kama utapata la 2nd au 3rd Generation lile ndio tamu zaidi kwa mwanamke. Ile first generation limekaa kiume sana
 
Kazi unayo.
 
Asee ebu acha kulinganisha ujinga na forester asee.

Kwanza Forester iko economic way more ukilinganisha na kluger. Then ukija kwenye look (facial impression[emoji16][emoji5])..agh hata tusiongee forester takes it all. Perfomance sasa ndo sitaki kuweka neno maana inajulikana forester ni kinara.

Note! This is all about forester za kuanzia 2009). The only negative thing about forester ni spares though ukishafunga ndo mmemalizana hivo japo prices za spare zimechangamka kidogo.
 
RRONDO hebu tia neno hapa: Forester vs Kluger, mambo ya wana ndoa tuwaachie wenyewe wanajuana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…