Subira Yangu - Nyota Ndogo

Subira Yangu - Nyota Ndogo

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi kuna wapenzi wengine wa Nyota Ndogo humu jamvini?

Nampenda sana huyu mdada kutoka Mvita.

Nampenda kuhusu mengi [ila msiniulize mengi yepi...jiongezeni wenyewe].

Anaonekana ni mdada maridhia kabisa na ikitokea bahati ya kukutana naye basi kwangu litakuwa ni jambo la adhama kubwa.

Huu wimbo wake mpya nimetokea kuupenda sana.

Nimeupa nyota sita kati ya tano.

Pia ujumbe wake ni murua kabisa. Unafaa kwenye miktadha mbalimbali ya mapitio ya kimaisha.

Furahia.

Huyu dada ana kipaji kikubwa cha kuimba.

Hiki kipaji angejaaliwa Jike Shupa(Shilole) na kile kizungu chake cha Igunga nahisi tungepata tabu sana tusiomkubali.
 
Niliupenda sana ule wimbo wake wa Kuna watu Na Viatu Duniani. Ila mdada anajitahidi sana
 
Hivi kuna wapenzi wengine wa Nyota Ndogo humu jamvini?

Nampenda sana huyu mdada kutoka Mvita.

Nampenda kuhusu mengi [ila msiniulize mengi yepi...jiongezeni wenyewe].

Anaonekana ni mdada maridhia kabisa na ikitokea bahati ya kukutana naye basi kwangu litakuwa ni jambo la adhama kubwa.

Huu wimbo wake mpya nimetokea kuupenda sana.

Nimeupa nyota sita kati ya tano.

Pia ujumbe wake ni murua kabisa. Unafaa kwenye miktadha mbalimbali ya mapitio ya kimaisha.

Furahia.

Mimi nimependa wewe ulivyotumia kiswahili fasaha kwa kuweka misamiati mahala panapostahili.
 
Nitumie whatsapp namba angu ni 0765373363
 
Shukran NN kwa kunikumbusha huyu nyota ndogo mimi nilianza kumkubali katika wimbo wa nibebe pale alinibeba kweli kwa ule utunzi wake ukija ule wa kuna watu na viatu acha niweke wazi nami namkubali sana kwa tungo zake mahiri.
 
Back
Top Bottom