Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 16
- 16
Serikali ya Sudan Kusini imetoa agizo la kuzuia upatikanaji wa mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook na Tiktok nchini humo kwa muda wa hadi miezi mitatu, huku ikitegemea udhibiti wa maudhui.
Agizo hilo limetolewa na Mamlaka ya Kitaifa ya Mawasiliano ya Sudan Kusini (NCA) Jumatano Januari 22, 2025, huku likitajwa kusababishwa na video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ikionyesha wakimbizi wa Sudan Kusini wakishambuliwa na watu wanaosemekana kuwa wanajeshi wa Sudan.
Akizungumzia agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NCA, Napoleon Adok amesema; "Tunaomba rasmi kuzuiwa kwa tovuti hizi za vyombo vya habari kwa angalau siku 30. Agizo hili linaweza kuondolewa mara tu hali itakapodhibitiwa. Maudhui yanayoonyeshwa yanakiuka sheria zetu za ndani na yanahatarisha usalama wa umma na afya ya akili, hasa vikundi vilivyo hatarini.”