Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini, amembadilisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, ikiwa zimesalia takribani miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu wa kwanza nchini humo tangu kupata uhuru mwaka 2011.
Taarifa hiyo ililosomwa Septemba 15 na chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali limemtaja Katibu Mkuu wa Tume hiyo, Gabriel Bol Deng, kuwa mrithi wa Abednego Akok Kacuol. Rais Kiir hakutoa sababu ya mabadiliko hayo.
Sudan Kusini imekuwa katika hali ya amani tangu makubaliano ya mwaka 2018 yalipomaliza vita vya miaka mitano vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu. Hata hivyo, bado kuna matukio ya mara kwa mara ya vurugu kati ya jamii mbalimbali.
Uchaguzi wa Rais na Wabunge umepangwa kufanyika Desemba 22.
Edmond Yakani, Mkurugenzi Mtendaji wa Community Empowerment for Progress Organisation la kundi la Wnaharakati wa Sudan Kusini, amesema mabadiliko hayo yanayofanyika karibu na uchaguzi yanaweza kupunguza imani ya wapiga kura.
"Kumwondoa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi miezi mitatu kabla ya uchaguzi ni janga, na hili linaenda sambamba na swali la viongozi wa kisiasa wanafikiria nini kuhusu uchaguzi huo,” amesema Yakani akizungumza na Reuters.
Hvi karibuni, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini ilisema nchi hiyo bado haina mifumo ya kutosha ya kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi wa amani na unaoaminika.
==============
South Sudan’s President Salva Kiir has replaced the head of the election commission, only about three months before the first national election since independence in 2011.
The president, in an announcement read out by the state-owned broadcaster on Tuesday, said commission Secretary General Gabriel Bol Deng will replace Abednego Akok Kacuol. He gave no reason for the change.
South Sudan has been at peace since a 2018 agreement ended a five-year conflict during which thousands of people were killed. Still, inter-communal violence is frequent.
Presidential and parliamentary elections are scheduled for December 22.
Edmond Yakani, executive director of Community Empowerment for Progress Organisation, a South Sudan activist group, said the replacement this close to the election risks eroding voter confidence.
“Firing a chairperson of an electoral commission three months before the election is a disaster, but this goes together with what is the political leadership thinking about the elections,” he told Reuters.
Last week, the United Nations Commission on Human Rights in South Sudan said the country lacked safeguards and conditions for peaceful and credible elections.
Source: Reuters & CNBC