Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi mkuu mpaka 2026

Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi mkuu mpaka 2026

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Serikali ya Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 2024 hadi Desemba 2026 kutokana na changamoto za maandalizi. Ofisi ya Rais Salva Kiir imetaja hitaji la muda zaidi kukamilisha sensa, uandishi wa Katiba mpya, na usajili wa vyama vya siasa.

Uchaguzi huo umeahirishwa mara ya pili, huku serikali ikikabiliwa na matatizo ya kiuchumi na changamoto za utekelezaji wa mkataba wa amani wa 2018 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Kiir na makamu wake, Riek Machar, wanataka kutimiza masharti ya mkataba huo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom