Sudan: Wananchi wapinga Utawala wa Kijeshi

Sudan: Wananchi wapinga Utawala wa Kijeshi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Makundi ya kutetea demokrasia ya Sudan yameanzisha mgomo na kutofuata sheria Jumapili ikiwa ni hatua ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Washiriki walionekana wachache kwa sababu ya kuendelea kuzuiwa kwa mtandao wa internet na mawasiliano ya simu.

Kamati ya mgomo, na chama cha wataalamu wa Sudan (SPA) ambacho kiliongoza maandamano yaliyo muondoa Omar Al-Bashir mwezi Aprili 2019, ndio wanaandaa maandamano ya kujaribu kuiondoa serkali ya kijeshi.

Watu walitoka nje Jumapili kwenda mitaani katika mji mkuu wa Khartoum, licha ya kwamba kulikuwa na watu wachache kwa kumibu wa wakazi.

Wanachama wa chama cha waalimu wamesema kwamba vikosi vya usalama vilitumia gesi ya machozi kuzuia mkutano uliokuwa ukifanyika katika jengo la wizara ya elimu mjini Khartom, ulikuwa na lengo la kupinga makabidhiano yoyote na utawala wa kijeshi.

Watu 87 walikamatwa kwa mujibu wa chama cha waalimu.

VOA Swahili
 
Back
Top Bottom