The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Wakati Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir akifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu nje ya nchi baada ya miaka mingi ya uvumi kuhusu afya yake, wachambuzi wanasema kuna mpango wa muda mrefu kuhakikisha urithi wake.Bw. Kiir alirejea siku ya Jumatano kutoka Falme za Kiarabu. ambapo aliikaa kwa angalau siku 10. Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kwamba "alikuwa anachunguza njia mpya za ushirikiano wa kiuchumi."
Lakini wasaidizi wake, wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, hapo awali waliliambiashirika la habari la AFP kwamba alikuwa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya kimatibabu, na kutilia mkazo wasiwasi wa muda mrefu kuhusu afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73.
Sudani Kusini ambayo ni chi changa zaidi duniani, imekumbwa na umaskini na ghasia tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2011, vikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu wapatao 400,000 kati ya mwaka 2013 na 2018.
Baada ya miaka michache ya utulivu wa kiasi, nchi hiyo ilitumbukia tena katika machafuko katika miezi ya hivi karibuni, yaliyozushwa, wachambuzi wanasema, kutokana na kuzorota kwa afya ya Kiir na juhudi zake za kumtangaza mrithi wake, mfanyabiashara Benjamin Bol Mel.
Bol Mel ni mtu mwenye utata, ambaye alipata umaarufu kama mkuu wa ujenzi na anajulikana kwa kusimamia fedha za familia ya Kiir.
Aliwekwa kwenye orodha ya vikwazo vya Marekani mwaka 2017 kwa rushwa.
Kwa miezi kadhaa, Kiir amekuwa akifanya ujanja wa kuwaweka kando wapinzani wake.