Sudani Kusini: Rais Kiir amfukuza kazi Gavana wa Benki kuu ya nchi hiyo

Sudani Kusini: Rais Kiir amfukuza kazi Gavana wa Benki kuu ya nchi hiyo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemfuta kazi Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo, Johnny Ohisa, katika hatua ya karibuni ya mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanywa ndani ya serikali yake.

Kiir alitangaza uamuzi huo usiku wa Julai 29, 2026 kupitia amri iliyosomwa na shirika la utangazaji la serikali, bila kueleza sababu za kumwondoa Ohisa.

Kwa sasa, uchumi wa Sudan Kusini unakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwemo kupungua kwa mapato ya mafuta, uhaba wa fedha taslimu, mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu ya taifa.

Nafasi ya Ohisa imechukuliwa na Addis Ababa Othow, ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu kuanzia Juni hadi Novemba mwaka 2025.

Katika miezi ya hivi karibuni, Rais Kiir amefanya mabadiliko kadhaa kwa viongozi waandamizi serikalini.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaamini hatua hizo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ushawishi wake wa kisiasa wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu suala la urithi wa uongozi nchini humo.

1785405691257.png

Soma pia

=============

South Sudan’s President Salva Kiir has dismissed the country’s central bank governor, the latest in a series of sackings and reshuffles in senior ranks of his government.

Kiir announced the removal of Johnny Ohisa late on Wednesday.

South Sudan’s economy has faced mounting pressure from declining oil revenues, recurring cash shortages, high inflation and currency depreciation.

Kiir, who did not give a reason for the sacking in the decree read on the state broadcaster, replaced Ohisa with Addis Ababa Othow, who held the same position between June and November last year.

In recent months Kiir has made a series of sweeping changes in senior ranks of his government, which analysts say signal an effort to consolidate power amid succession uncertainty.

Ohisa, an economist who has served multiple terms as central bank governor in the past, was reappointed earlier this year after previously holding the position on two separate occasions.


Source: CNBC AFRICA
 
Back
Top Bottom