Sufuria mpya haiivishi ugali, kwanini?

Sufuria mpya haiivishi ugali, kwanini?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Jamani, nimejaribu mara kadhaa kupika ugali kwa kutumia sufuria mpya, mara zote ninatoa ugali wa ajabu, na mimi ni mzoefu wa kupika ugali. Nikishapikia chakula kingine na kupikia tena ugali sufia ili, mambo yanakuwa mswano. Kuna aliyekumbana na hili?
 
sufuria za aina gani hizo??....
 
Mmmh ,cdhani kama kuna ukwer (labda) , ngoja waje wazoefu wa kupika
 
Kuanzia zile wanazopitisha wamachinga mpaka none stick zote jibu moja.
sijui sababu za kisayansi nyuma yake,lakini nadhani naweza kutoa sababu za kisaikolojia (Mtazamo wako juu ya kupika Ugali katika sufuria mpya).Yaani ule ''mshawasha'' na ''udambwi udambwi'' wa kupikia sufuria mpya,pengine unapunguza ufanisi wako katika pishi hilo.Mi nadhani hivyo,labda si sahihi..
 
Si elewi kwani nyanya yangu aliniusia kabisa kuwa kuwa ugali unahitaji moto mkali amasivyo utainama, hata moto uwe mkali kwa sufuria mpya ninaishia kupata ugali uliyoinama.
 
Jamani, nimejaribu mara kadhaa kupika ugali kwa kutumia sufuria mpya, mara zote ninatoa ugali wa ajabu, na mimi ni mzoefu wa kupika ugali. Nikishapikia chakula kingine na kupikia tena ugali sufia ili, mambo yanakuwa mswano. Kuna aliyekumbana na hili?
Nialike nije kushuhudia maana mimi ni Tomaso
 
Jamani, nimejaribu mara kadhaa kupika ugali kwa kutumia sufuria mpya, mara zote ninatoa ugali wa ajabu, na mimi ni mzoefu wa kupika ugali. Nikishapikia chakula kingine na kupikia tena ugali sufia ili, mambo yanakuwa mswano. Kuna aliyekumbana na hili?

Kwa sababu Ugali siyo chakula bali ni pumba!
 
Maganjo wa Uganda au Iwisa wa South Africa na Azam siku nyingine lakini ninapenda sana Maganjo.
uganda wana mahindi mazuri kweli? ugali wa malawi mtamu sio mzuri au wa zambia yaani unaweza kula debe
 
Back
Top Bottom