Suge Knight anasema 2Pac hajafa!!

Suge Knight anasema 2Pac hajafa!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
Katika pitapita nikakuta blog ya Sammisago akiwa ameandika hii story
===============================
Suge Knight asema hana imani kuwa 2 Pac amekufa

Share Habari Na Marafiki Zake
Kwenye Interview ndefu itakayoruka weekend hii nchini Marekani ikiwa na ushahidi mpya kuhusu kifo cha 2 Pac, mmiliki wa Death Row Records Suge Knight amesema hana uhakika kama 2 Pac amekufa.

Suge ambaye alikuwa kwenye gari wakati 2 Pac anapigwa risasi amesema kwenye interview na Ice T na mwandishi Soledad O’Brien “Nilipoondoka Hospitalini baada ya 2 Pac kuhudumiwa kutokana na kupigwa risasi, alikuwa powa tu na tulitaniana na kucheka, Sioni jinsi gani mtu anaweza badilika hali kutoka kuwa na nafuu mpaka kuwa na hali mbaya kabisa”

Akaulizwa Je 2 Pac Yuko hai, alijibu> Nakwambia, Jinsi alivyo 2 Pac, huwezi kujua.

Interview hii inaitwa “Who Shot Biggie & Tupac?” itaruka Jumapili hii ikiongelea mauwaji ya wasanii wakubwa wa hiphop Christopher “The Notorious B.I.G.” Wallace na 2Pac.

Shakur alifariki Sept. 13, 1996 baada ya kupigwa risasi mjini Las Vegas na Wallace alifariki March 9, 1997 baada ya kupigwa risasi mjini Los Angeles.

Waliofanya mauwaji haya hawajawahi kukamatwa.

Suge Knight asema hana imani kuwa 2 Pac amekufa – Home-Sammisago.Com
 
Huwa najiuliza kwa nini kifo cha 2pAc kina mashaka yaani wengi tumekuwa wagumu kuamini juu ya kifo chake.. Mbona hakuna utata wowote juu ya notorious b.i.g!? Kama yuko hai au amekufa?.. Au tupac hakustahili kufa!? ifike wakati tuamini tu kuwa kifo kinamuhusu kila kiumbe chenye uhai.. Sisi ni mali ya mungu. RIP 2pac na big
 
Huyu Suge ameshaongea vitu tofauti huko nyuma tena sio mara moja, kwahiyo sijui kama watu watamchukulia serious anymore.
 
Huyo Sugu kinight anatusaidia nini kwenye Tanzania ya Viwanda na kuisoma namba?
Linapokuja suala la kufananisha na kutofautisha ndio sehemu pekee ya kutambua akili ndogo na kubwa. Inamaana umeshindwa kutofautisha maudhui ya kila jukwaa hapa jf mpaka kufikia kiwango cha kujizalilisha kiasi hichi. Kuuonyesha ujinga wako hadharani haijawahi kua sifa nzuri.
 
Mungu kaumba sahau kwenye kifo, ndio maana ni rahisi MTU kusahaulika

Ukiona MTU kafa na miaka zaidi ya 20 imepita na bado watu wanahofu huenda kweli hajafa
 
Hey brothers!..2pac sio mtu
2pac ni taasisi ambayo milele haiwezi kufa..

Omar Shakur yeye ameshakufa
na alitabiri kifo chake na itachukia muda sana Dunia kukubali kwamba hayupo.

Kuna watu wanadai yupo Cuba, Pueto Rico au kwenye visiwa Latin America ila sio kweli.

Mwandishi mmoja aliyekuwa maarufu wakati 2pac anafanya vizuri aliwahi kusema kwamba anavyomjua 2pac angekua hai leo asingeweza kunyamaza kimy fake rappers kama Drake, Meek Meel na Rick Ross waisumbue dunia lazima angetoka kiwadiss

Omar is gone we should keep sail and stay with 2pac's 'lyrics and princples because that will stay with us Foever.

Ain't mad at cha &
Dear Mama
My most Favourite; )
 
MJINGA..
Linapokuja suala la kufananisha na kutofautisha ndio sehemu pekee ya kutambua akili ndogo na kubwa. Inamaana umeshindwa kutofautisha maudhui ya kila jukwaa hapa jf mpaka kufikia kiwango cha kujizalilisha kiasi hichi. Kuuonyesha ujinga wako hadharani haijawahi kua sifa nzuri.
 
Hey brothers!..2pac sio mtu
2pac ni taasisi ambayo milele haiwezi kufa..

Omar Shakur yeye ameshakufa
na alitabiri kifo chake na itachukia muda sana Dunia kukubali kwamba hayupo.

Kuna watu wanadai yupo Cuba, Pueto Rico au kwenye visiwa Latin America ila sio kweli.

Mwandishi mmoja aliyekuwa maarufu wakati 2pac anafanya vizuri aliwahi kusema kwamba anavyomjua 2pac angekua hai leo asingeweza kunyamaza kimy fake rappers kama Drake, Meek Meel na Rick Ross waisumbue dunia lazima angetoka kiwadiss

Omar is gone we should keep sail and stay with 2pac's 'lyrics and princples because that will stay with us Foever.

Ain't mad at cha &
Dear Mama
My most Favourite; )
Omar Shakur ndio nani tena?
 
Back
Top Bottom