Sugu achana naye kabisa, Mbunge anayenesa na michango ya HipHop

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Bila shaka unamfahamu Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Huyu jamaa ni mmoja kati ya wanamuziki wakongwe nchini, ameanza kuimba nyimbo za Bongo Fleva tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Moja ya nyimbo zake ni ule wa ‘ana miaka chini ya 18’, ambao unamuelezea binti mwenye umri chini ya miaka 18 ambaye alirubuniwa na wanaume na kujikuta akiwa na watoto wawili ambao baba zao hawajui.

Nyimbo alizokuwa akiimba katika majukwaa sasa amezihamishia bungeni.

Huwa akisimama kuchangia hoja mbalimbali kwanza huzungumza kama yupo jukwaani vile, huku akichomekea maneno ya Kiingereza kuweka msisitizo. Amekuwa mtamu kwelikweli siku hizi.
Kali zaidi ni jinsi anavyotembea, miondoko yake ni kama ananesanesa hivi. Si umewahi kumuona akiwa jukwaani? Basi kama hujawahi kumuona subiri kampeni zianze.
‪
 



hili ndio tatizo la kutupelekea vilaza bungeni, badala ya kupambana kwa hoja wanapeleka ubaunsa bungeni
 
Teh Teh huyu jamaa bangi sana ukichanganya na yule mchumba wake mvaa pampas ni vituko tupu..
 
Ha ha ha JF bhana fulu burudani,mimi nasubili swaga za shishi baby,nasikia naye atagombea jimbo moja Tabora..
 
2015 tutaanzisha group la bunge flava, Sugu ndani, afande sele, Prof J, shilole, vicky kamata, Na nani mwengine Hebu ongezea watia nia hapo na kingwendu kweli na Juma nature kiroboto
 
2015 tutaanzisha group la bunge flava, Sugu ndani, afande sele, Prof J, shilole, vicky kamata, Na nani mwengine Hebu ongezea watia nia hapo na kingwendu kweli na Juma nature kiroboto

Nmeskia wema atagombea kwa mwigulu kupitia ccm akat mwugulu akigombea urais
 
alisema hivi...namnukuu
"men liar...women liar...but number dont lie"...mwisho wa kunukuu
big up sugu somehow umejenga confidence sasa.
 

Sio vibaya wala dhambi ukisema umenukuu kwa mtu fulani ama chombo Fulani cha habari.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…