Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,860
Bila shaka unamfahamu Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi Sugu. Huyu jamaa ni mmoja kati ya wanamuziki wakongwe nchini, ameanza kuimba nyimbo za Bongo Fleva tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Moja ya nyimbo zake ni ule wa ana miaka chini ya 18, ambao unamuelezea binti mwenye umri chini ya miaka 18 ambaye alirubuniwa na wanaume na kujikuta akiwa na watoto wawili ambao baba zao hawajui.
Nyimbo alizokuwa akiimba katika majukwaa sasa amezihamishia bungeni.
Huwa akisimama kuchangia hoja mbalimbali kwanza huzungumza kama yupo jukwaani vile, huku akichomekea maneno ya Kiingereza kuweka msisitizo. Amekuwa mtamu kwelikweli siku hizi.
Kali zaidi ni jinsi anavyotembea, miondoko yake ni kama ananesanesa hivi. Si umewahi kumuona akiwa jukwaani? Basi kama hujawahi kumuona subiri kampeni zianze.
‪