SUGU adai yeye ndiye muasisi wa Bongofleva

SUGU adai yeye ndiye muasisi wa Bongofleva

BONGO FLEVA NI STORY YA SUGU, MIKE NA TAJI

JOSEPH Mbilinyi ‘2 Proud’, kazi yake “Ni Mimi" ndio wimbo wa kwanza wa Swahili Rap kusikika Radio One Stereo mwaka 1994. Vilevile akawa Rapper wa kwanza wa Swahili Rap kufanya mahojiano Radio One.

Mike Mhagama, alikuwa mtangazaji wa kwanza kugonga ngoma ya Swahili Rap. Mmiliki wa wimbo alikuwa 2 Proud a.k.a Mr II au kwa uzito zaidi mwite Sugu.

Taji Liundi ‘Master T', ndiye mtayarishaji wa kwanza wa shoo za Swahili Rap. Akawa DJ wa kwanza Bongo kucheza nyimbo za Swahili Rap. Akaasisi kipindi cha DJ Show, Radio One, kilichopiga ngoma mfululizo za Kiswahili.

TUMENG'ENYE STORY

Mike alipiga ngoma ya Sugu “Ni Mimi". Mdundo kwenye spika za radio, ukatema “nipo kwenye microphone, hata unipe nini sitamani sioni, Ni Mimi". Uthubutu wa kucheza wimbo huo nusura umletee balaa kazini.

Sera ya Radio One haikuruhusu Swahili Rap kuchezwa redioni kabisa. Big Boss Julius Nyaisanga, alimuibukia Mike studio, kumtamka ajieleze kwa nini amecheza wimbo wa Sugu kinyume na sera ya taasisi?

Nyaisanga alipoingia studio, akamkuta Mike anapata wakati mgumu kujibu simu nyingi za wasikilizaji waliotaka wimbo wa Sugu urudiwe. Watu walifurahia uthubutu wa Mike. Walipenda wimbo wa Sugu kupigwa redioni.

Nyaisanga akaona hakuna budi, akamruhusu Mike arudie kuucheza wimbo Ni Mimi wa Sugu. “Huwezi kuzuia mvua, Sugu ni mvua kama inanyesha inanyesha" – Sugu!

Wimbo ulichezwa, ukarudiwa na kurudiwa, ikabidi Sugu aitwe kwa ajili ya mahojiano redioni. Demand ilikuwa kubwa.

Master T ‘Taji', akairasimisha Swahili Rap kupitia DJ Show ya Radio One. Ni kupitia DJ Show, mwaka 1996, Mike akaanza kuita Swahili Rap kwa jina la Bongo Fleva.

Hivyo, ukisikia jina “Bongo Fleva”, ujue kuna mahali limetoka. Wimbo “Ni Mimi” wa Sugu uliwapa sababu Mike na Taji kuipigania Swahili Rap kwenye vyombo vya mawasiliano ya umma, kisha jina la Bongo Fleva likazaliwa.

Mei 31, ni siku ya “The Dream Concert”, Sugu atafanya shoo “presidential” Serena Hotel, kuadhimisha miaka yake 30 kwenye game. Mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan. Taji ndiye MC. Mike yupo Marekani anacheza na Benjamins.

Kutoka muziki usioruhusiwa kusikika redioni hadi kuwa sanaa ya heshima na Rais anakuwa mgeni rasmi, ni safari ndefu, ilikuwa kama ndoto lakini sasa ni halisi. Twen'zetu Serena. The Dream Concert.
Kweli concert lina haki ya kuitwa the dream concert
 
Na huyu ndio alitoa albam ya kwanza ya rap kabla ya kina sugu ilikuwa na nyimbo sita kabla redio one haija anzishwa tulipiga donee tukainunua pale lang'ata ilikuwa inauzwa 600,dah kitambo sana

Alikuwepo Saleh Jabir,huyu alikua ana rap Kiswahili japo kwa kuchukua midundo ya nyimbo za watu,kama ule wimbo wa Vanilla Ice.
 
"Niko mikononi mwa polisi maisha yangu ni mikosi afandeeeeee!!!!* Aisee
 
Wimbo wa kwanza wa rap wa kiswahili kuwa mainstream ulikuwa wimbo wa Nigga J, Chemsha Bongo.
*Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa,maisha nimechezea leo hii nalala njaa chemsha bongo kabla hujapagawa utashangaa chemsha bongo kabla hujapawa utaduwaa

Kwa kifupi nilikulia kwenye maisha ya kitajiri..wazazi walinipenda walinipa hili na lile

Na kila slinighasi aliozea segerea!!!*[emoji445][emoji445]
 
Legendary wa Muziki Nchini Tanzania na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a k a Mr.Sugu,amejigamba kwamba yeye ndio jasiri muongoza njia wa Muziki hapa Tanzania na kwamba ndiye aliwafungulia njia ya Mafanikio Wasanik wote..

Aliyasema hayo hivi karibuni katika tamasha la Dream Concert aliloliandaa Serena hotel kusherekea birthday ya miaka 50 na mafanikio kwenye sekta ya Muziki Tanzania..

Miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la Sugu alikuwa Rais wa JMT,mh.SS Hassan..

Hongera bwana Sugu 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220603-104936.png
    Screenshot_20220603-104936.png
    140.1 KB · Views: 26
Back
Top Bottom