Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh umezaliwa mwaka gani [emoji3][emoji3]Wimbo wa kwanza wa rap wa kiswahili kuwa mainstream ulikuwa wimbo wa Nigga J, Chemsha Bongo.
Dully anaanza muziki, watu tumeshaanza kuruka ngoma za 11 proud zamani.Dully kaanza lini muziki?Muasisi wa bongofleva aka baibuda ni Dully Sykes.
Muasisi wa Swahili rap ni Saleh Jabir.
Jifunze huu muziki vizuri.
Vipi kwanza unit mkuu.
Kuna ule wimbo wa sijui lini nitafika mpaka leo naukubali kinoma.
Nakutana shetani anauliza we nani na unataka nini, njoo unifuate mimi. Dah miss those old days
Kuna ile alitembea nayo marehemu D rob inaitwa 'nakuja' sec version,kama unayo hebu iweke nayo hapa Mwl😃
Vp kuhusu Salehe Jabiri...sugu ache sifa zisizo zakeBONGO FLEVA NI STORY YA SUGU, MIKE NA TAJI
JOSEPH Mbilinyi ‘2 Proud’, kazi yake “Ni Mimi" ndio wimbo wa kwanza wa Swahili Rap kusikika Radio One Stereo mwaka 1994. Vilevile akawa Rapper wa kwanza wa Swahili Rap kufanya mahojiano Radio One.
Mike Mhagama, alikuwa mtangazaji wa kwanza kugonga ngoma ya Swahili Rap. Mmiliki wa wimbo alikuwa 2 Proud a.k.a Mr II au kwa uzito zaidi mwite Sugu.
Taji Liundi ‘Master T', ndiye mtayarishaji wa kwanza wa shoo za Swahili Rap. Akawa DJ wa kwanza Bongo kucheza nyimbo za Swahili Rap. Akaasisi kipindi cha DJ Show, Radio One, kilichopiga ngoma mfululizo za Kiswahili.
TUMENG'ENYE STORY
Mike alipiga ngoma ya Sugu “Ni Mimi". Mdundo kwenye spika za radio, ukatema “nipo kwenye microphone, hata unipe nini sitamani sioni, Ni Mimi". Uthubutu wa kucheza wimbo huo nusura umletee balaa kazini.
Sera ya Radio One haikuruhusu Swahili Rap kuchezwa redioni kabisa. Big Boss Julius Nyaisanga, alimuibukia Mike studio, kumtamka ajieleze kwa nini amecheza wimbo wa Sugu kinyume na sera ya taasisi?
Nyaisanga alipoingia studio, akamkuta Mike anapata wakati mgumu kujibu simu nyingi za wasikilizaji waliotaka wimbo wa Sugu urudiwe. Watu walifurahia uthubutu wa Mike. Walipenda wimbo wa Sugu kupigwa redioni.
Nyaisanga akaona hakuna budi, akamruhusu Mike arudie kuucheza wimbo Ni Mimi wa Sugu. “Huwezi kuzuia mvua, Sugu ni mvua kama inanyesha inanyesha" – Sugu!
Wimbo ulichezwa, ukarudiwa na kurudiwa, ikabidi Sugu aitwe kwa ajili ya mahojiano redioni. Demand ilikuwa kubwa.
Master T ‘Taji', akairasimisha Swahili Rap kupitia DJ Show ya Radio One. Ni kupitia DJ Show, mwaka 1996, Mike akaanza kuita Swahili Rap kwa jina la Bongo Fleva.
Hivyo, ukisikia jina “Bongo Fleva”, ujue kuna mahali limetoka. Wimbo “Ni Mimi” wa Sugu uliwapa sababu Mike na Taji kuipigania Swahili Rap kwenye vyombo vya mawasiliano ya umma, kisha jina la Bongo Fleva likazaliwa.
Mei 31, ni siku ya “The Dream Concert”, Sugu atafanya shoo “presidential” Serena Hotel, kuadhimisha miaka yake 30 kwenye game. Mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan. Taji ndiye MC. Mike yupo Marekani anacheza na Benjamins.
Kutoka muziki usioruhusiwa kusikika redioni hadi kuwa sanaa ya heshima na Rais anakuwa mgeni rasmi, ni safari ndefu, ilikuwa kama ndoto lakini sasa ni halisi. Twen'zetu Serena. The Dream Concert.
Vp kuhusu Salehe Jabiri...sugu ache sifa zisizo zake
Dully kaanza kwenda mainstream 1999 enzi za JulietaDully anaanza muziki, watu tumeshaanza kuruka ngoma za 11 proud zamani.Dully kaanza lini muziki?
Unaijua bongofleva lakini wewe? Sugu haimbi bongofleva Dully ndio mwanzilishi wa bongofleva au jina lingine inaitwa baibuda Sugu pia hata Swahili rap hakuanzisha yeye aliyeanza kurap kwa Kiswahili ni Saleh JabirDully anaanza muziki, watu tumeshaanza kuruka ngoma za 11 proud zamani.Dully kaanza lini muziki?
Wakati huo radio ilikuwa moja tu radio tanzania. Saleh Jabir alikuwa na album na iluzwa mpaka madukani. Hata GWM wameanza kurap Kiswahili kabla ya Sugu.Tatizo hakukua na kumbukumbu, Naomba nisaidie aliimba kiswahili na zilikua zinapigwa redioni? Maana mtu akirekodi akakaa na tape ndani ni ngumu kufahamika
Sidhani kama wana undugu nachofahamu Saleh Jabir ana udugu na Salama Jabir.Saleh jabir ana uhusiano gani na jabir saleh wa efm
Wewe ulikuwa bado kinda....siyo lazima kila uzi uchangie.Huwa naona kama jamaa anakuwa overrated sana. Binafsi sioni kipaji pale.
Saleh jabir alikuwa anafanya cover za nyimbo za mbeleVp kuhusu Salehe Jabiri...sugu ache sifa zisizo zake
Hawa watoto wanaupeo mdogo sana mfano aliyeanzisha hip hop ni yule jamaa wa Bronx lakin jamaa hakua mkali kivile lakin awali ni awali tuWatoto wa juzi hamuwezi kuelewa, uasisi ni tofauti na hicho unaita kipaji.
Na ule Ana miaka chini ya 18 ,sijui waitwaje!Nyimbo ziljaa jumbe nzuri,ziliasa jamii ,zilisuta ,zilifundisha ,zilitoa burudani..
"Niko mikononi mwa Polisi.....Afandeee" mmoja ya kibao bora kabisa toka kwa mkongwe huyo.