Sugu amvaa Kihongosi, amtaka aachane na Heche

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Your browser is not able to display this video.

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu), amemtaka Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, kuacha kumzungumzia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, katika mikutano yake ya hadhara.

Soma pia: Kihongosi amshambulia Heche, CHADEMA katika ziara ya Dar es Salaam

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kirando, Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, Septemba 20, 2026, Sugu amesisitiza kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kujikita katika kueleza utekelezaji wa ahadi zao kwa wananchi badala ya kutumia mikutano ya hadhara kuwashambulia na kuwazungumzia viongozi wa upinzani kama John Heche.
 
"Kujikita katika kutekeleza ahadi zao" Naunga mkono hoja hii..CCM walituahidi ndani ya siku 100 kuanza kwa mchakato wa "KATIBA MPYA"..Huo mchakato unaanza lini?Na kipi kilikwamisha? na KATIBA MPYA inapatikana lini? Na kwanini mpaka sasa haijapatika? maana kabla ya 2030 tuwe katika nyumba mpya. Samahanini CCM nina familia, nawakumbusha Ahadi yenu wenyewe .Wahenga walisema "Ahadi ni Deni" kwahiyo, Mnadeni kwa wananchi na msipo lilipa mjiandae maswali 2030. KIHONGOZI aione hii kwenye jalada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…