carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa kimesema kinafuatilia taarifa za kuchukuliwa kwa Katibu wake wa Kanda hiyo, Grece Shio, ambaye inadaiwa alichukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwao Kimara, Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi, imeeleza kuwa familia ya Shio ndiyo iliyomfikishia taarifa hiyo, huku hadi wakati wa kutolewa kwa taarifa hiyo kukiwa hakuna maelezo kuhusu kituo alikokuwa akishikiliwa au kosa linalohusishwa na kukamatwa kwake.
Mbilinyi amesema amewasiliana na mawakili wa chama hicho, Dickson Matata na Hekima Mwasipu, ili kusaidia kufuatilia suala hilo na kubaini alipo Shio pamoja na sababu za kuchukuliwa kwake.
Chanzo: Royal Tv