- Source #1
- View Source #1
Wakuu hii ni kweli?
- Tunachokijua
- Joseph Mbilinyi (Sugu) ni Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa ambaye amewahi pia kuwa mbunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la mbeya mjini.
Madai
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii Julai 11, 2025 wamechapisha taarifa iliyoambatana na grafiki ikieleza kuwa Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) amechapisha taarifa katika ukurasa wake wa X akieleza kuwa maamuzi ya kutoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ni ya watu wachache na sio wa chama.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na utafutaji wa maneno muhimu umebainisha kuwa pichaskrini (sreenshot) inayoonesha taarifa kutoka ukurasa wa X ikiwa imechapishwa na Sugu ni ya kughushi kwani haijachapishwa na yeye katika ukurasa wake rasmi.
Katika ukurasa wake wa X, Sugu amekuwa akiunga mkono ajenda ya No reforms No election mathalani ujumbe wake aliouchapisha Julai 9, 2025 unaoashiria kuwa Mwenyekiti huyo wa Kanda bado anaiunga mkono ajenda hiyo.
“Hii AGENDA ya ‘ #NoReformsNoElection‘ pia imekaa Ki-HİP-HOP saaana…
NB: Ndio maana imebamba kila KONA!”
Grafiki zinazotumika kusambaza taarifa hiyo pia ni za kughushi kwani zimetumia aina tofauti ya mwandiko (fonts) ambayo ni tofauti na zinazotumiwa na chanzo na hazijachapishwa na vyanzo hivyo.