SUGU ATOA MAJIBU BUNGENI NA KUJILIZA MACHOZI……LOL..
MANGE 5 COMMENTS JUN 26,2015 UNCATEGORIZED
BASI SUGU NDO KAJIBU USHUZI HUU UFUATAO NA ALIVYOMALIZA KUTOA JIBU NA MCHOZI HUOOO,ETI KALIAAA…HAHAHA…NA KINACHOMLIZA MNADHANI NI NINI? NI AIBUUU NA SEKE SEKE ALILOLIPATA THE LAST 2 DAYS.HANA LOLOTE…. NA LINGINE LINALOMLIZA HAJUI UCHAGUZI UTAKUWAJE AKIWAZA KURUDI KUKATA VIUNI STEJINI NA BONGO FLAVA NDO MCHOZI UNAMTOKA…NA BADO….. YANI ASIMSUMBUE FAIZA KWENYE APPEAL TU….
"Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo"
"Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang'anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia"
"Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika"
"Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito"
"Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge"
"Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niiwashilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge"
"Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa" >>> Mbunge Joseph Mbilinyi.
Nimehighlight kwa red sehemu nilizoona ndo za kumjibia SUGU…
1. Kwanza Hili jibu la Sugu tu kwa Mh. Mlata linaonyesha kabisa jinsi alivyo ni mdhalilishaji wa wanawake….. Hivi kwanini aongelee ndoa ya Martha Mlata kuvunjika? Kwani Martha alimuattack kwa kuachana na Faiza au Shyrobe Banji na wengineo wengi mpaka aongee ndoa ya huyu mama bungeni? The only reason watu wamekuwa interested sana ni sababu hapa kuna issue ya mtoto mdogo pia sababu ya process nzima iliyotomika Faiza kupokonywa mtoto, na kumbuka watu wanamuona Faiza alivyo close na mtoto wake na anavyohangaika na mtoto wake ndo maana wakashangaa iweje anyang'anywe kisa nguo zake..Jamani embu tuongeee jamani naomba mmoja wetu aseme jamani mimi kweli niliwahi kupokonywa mtoto in 1 day! what kind of a custody case is this jamani? naomba kuuliza? Alafu zile process za kuanza ustawi wa jamii kabla hamjaenda mahakamni kwanini mahakama waliziruka kwa hii kesi ya Sugu? tunaomba clarifications hapa… Naomba kujua nani kawahi kusikia au kuona custody case ya 1 day only?? WHO?????? THATS ALL.
2. Kuhusu CHILD support hapo ukweli unaujua wewe na Faiza kila mtu ana lake, ila kwa shule mama mtu nasema kamlipia mtoto fee 3 times only. Na pesa yoyote ya child support ni mpaka Faiza aende kwa kaka yake akamlilie ndo kaka yake aongee na Sugu….
3. "Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge" – WHAT A SILLY MAN- HIKI ndo watu tunachokipinga na bado anakirudia tena. ETI MWANAMKE mnyonge anajulikana kumbi za starehe nchi nzima….Wewe mbona unajulikana nchi nzima kwa udhalilishaji wa wanawake. Na umeshasema mtoto toka kazaliwa analelewa na mama yake mpaka leo hii. Sasa kweli mavazi yake ndo useme hafai kuwa mama? Wewe Sugu isingekuwa unakimbia majukumu je uliwahi kumpa onyo mzazi mwenzio kuwa Faiza acha kuvaa hivyo? mbona hilo hujasema? Kama ungekuwa mstaarabu kama unavyojifanya si ungeongea na mzazi mwenzio kwanza kabla ya kwenda mahakamani. AU TUAMBIE kuwa jamani huyu mwanamke nimeongea nae mpaka nikachoka.Anauzi huyu baba jamani.
4.Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. – Sugu mbona umeruka ? mbona hujasema kuwa faiza alifika mahakamani bila kujua mmemutia nini wewe na huyo hakimu? Mbona hujasema mlimsave summons less than 24 hrs kabla hajatakiwa mahakani?kwanini hujaeleza kuwa jaji alichukua siku moja kutoa hukumu? mbona hujaeleza huko bungeni kuwa Faiza alimweleza hakimu kuwa wadogo zako wa damu wanaoishi na mama yako ambae umesema ndo atakuwa anakusaidia kulea mtoto walikuwa wanambaka housegirl mpaka housegirl kazaa mttoto humo humo ndani mwenu hajulikani ni wa kaka yupi? mbona haya hujaeleza bungeni ila uko fasta kueleza mavazi ya Faiza? ungeeleza yote ili kweli bungeni waone Faiza hafai? na hawa ndugu zako utawachukulia hatua????? maana its clear housegirl hawezi kukubali kulala na 2 brothers lazma walikuwa wanamkamata? tueleze kama mbunge hawa kaka zako watachukuliwa hatuwa gani kwa kumbaka housegirl? wanyanyasaji wakubwa wewe na ndugu zako .
5. mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Hahahahha, huna lolote eti umetoa nafasi majadiliani ya kifamilia yafanyike….Huna lolote wewe umeona nchi nzima wanawake wamekushikia kidete ndo maana hujaenda fata mtoto…. Ungekuwa unajua kuna kitu kama majadiliano ya kifamilia usingekimbilia mahakamani ,ungefanya kwanza haya majadiliano ya kifamia uone kama yatazaa matunda,ingeshindikana ndo ungeenda mahakamani.why ulianza mahakamni kwanza??? Faiza faiza nakurudia tena na nilijua tu Sugu atakujia na gia za maongezi ya kifamilia ili utulie. Usikubali usiache kesi.mwambie kwanza akurudishie custody ya mtoto ndo mfanye majadiliano ya kifamilia…..
6. MH. MARTHA MLATA – Huyu Sugu hana dili anajikosha kosha tu hapo bungeni tunaomba umuulize kama yeye anajua mambo private yawe ya kifamilia mahakamani alifata nini? kwani hakujua kuwa akienda mahakamani issue itakuwa public? si alijua? tatizo ni kwamba Sugu hakutugemea Faiza atapata support aliyoipata alidhani watu tutampuuzia Faiza na kusema bora sababu ya nguo zake ila alikosea mahesabu…. Anajifanya mtu wa maana embu muulize mbona mwanae SENEVA hamtakiiiii, kamtupa mpaka leo mtoto hajuani na baba yake??? Kweli vile tuongee vitu vya akili Sugu anamuona Faiza hafai Sugu ameshawahi hata kwenda shuleni kwa mwanae? anajuana hata na mwalimu mmoja wa mwanae? SHule ya mtoto inaitwajwe? aliulizwa mahakamani jina la shule ya mtoto hajui? akiulizwa mtoto kaumwa homa mara ngapi toka azaliwe hajui? kaharisha mara ngapi hajui? sababu mama mtu ndo anahangaika na mtoto…
JAMANI WABUNGE HUKO BUNGENI TUNAOMBA MUMCHACHAMLIE SUGU ISSUE YA MWANAE ALIEMTUMPA AANITWA SENEVA. EMBU AJIBU BASI KUHUSU HUYO MTOTO PIA. MBUNGE GANI ANATUPA MTOTO?
hahahhha
Jamani mimi kwa maoni yangu ka jinsi Sugu alivyoongea na kumalizia kwa kusema kuwa anataka wayamalize kifamilia na kumwaga mchozi ule basi naamini the worst is over na Faiza ataachwa na mwanae na Sugu haonekani kama mtu anaetaka kufight appeal ya Faiza.In short akili zimerudia baada ya kushikiwa viuno na wanawake wa kitanzania…hahahahaha….Kachoka na sisi mpaka mtoto kamwona mchungu maaan career ya ubunge ataikosa hivi hivi kwa hii kesi..hahahaha…. Tena ajitulize kabisaaa aaache appeal ipite kimya kimya na sie tumsahau….
Jamani tuendelee na shughuli zetu Sugu keshatusoma na katulia…. Faiza akituhitaji atatustua…
JAMANI WANAWAKE TUWE TUNASHIKAMANI HIVI ALL THE TIME MBONA WANAUME WATANYOOKA WOOTE….LOL…
UMOJA WA WANAWAKE OYEEEEEE!!
KWA VILE TUSHAMALIZANA NA ISSUE YA SASHA TUANZE NA YA SENEVA JAMANI MNAONAJE TUMFANYIE SUGU KAMPENI ATOKE BUNGENI????? MBUNGE GANI ANATUPA MTOTO WAKE ?
PS: Tuelewani nani alisema kuwa mtoto alikuwa keshabebwa???? ni kwamba Sugu alikuwa na right ya kumfata anytime na ndo maana watu tulicharuka kuwa afile appeal fastaaa maana appeal ikianza stop order inaweza kutolewa mpaka kesi iishe….