Tunashauriwa sana mambo ya ndoa kuishia ndani ya familia, yakishatoka nje ya familia matokeo yake ndiyo haya. Siri zote nje. Kwa hiki anachokisema Faiza naweza kukikubali kwa asilimia 70. Nakikubali kwa sababu kwa namna alivyo Faiza kimavazi na kimaneno inaakisi namna tabia ya Sugu ilivyo. Kwa mtu mstaarabu na anayesjiheshimu hakuna namna anaweza akaingia kwenye mahusiano na mtu kama Faiza acha tu mbali suala la kuzaa naye, hivyo Sugu alikuwa na tabia zinaondena na Faiza ndio maana alienda hata kujitambulisha nyumbani kwa akina Faiza na hata akaamua kuzaa naye. Haya yanayomtokea Sugu ni malipo ya uchafu aliokuwa anaufanya. Na bahati mbaya anaamua kuhangaika kujinasua kwenye hili janga la Faiza baada ya kujua yeye ni mbunge, na mbunge anapaswa kuwa na heshima fulani katika jamii. Huu ubaya wa Faiza anauona sasa hivi baada ya kuwa mbunge, na pengine baada ya wabunge wenzake kumsema kuwa anapaswa kuishi kama kiongozi wa jamii anayefuata maadili.