Diesel generator
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 706
- 661
huyu faiza ndiye Faizafoxy?
* Ishu sio mavazi tu...grounds za Sugu zilikuwa nne:
* Kuvaa mavazi ya nusu utupu, kupiga picha za nusu uchi na kuyatupia mtandaoni...
* Kumpiga mtoto picha mbaya ya kuyatupia humohumo mtandaoni...
* Kusafiri mda mrefu na kuwa mbali na mtoto...
* Kutokuwa na kipato cha kuweza kumlea mtoto...
Hapo kwenye kipato si angemuwezesha mama wa mtoto ili awe na uwezo wa kumlea binti....
Hili nalo neno
Ukutane na mtu club akiwa kavaa upaja nje azae nae halafu ategemee apige madera????
ukiongelea vazi tu mkuu naona hapana.... kuna watu wanavaa vizuri lakini hawana ulezi bora kwa watoto wao.... kwa kuangalia mavazi hukumu haijatenda haki... kuna kahali fulani cha kukomoana kipo
Angemuwezesha kivipi sasa?
Kwani yeye hawezi kutafuta shughuli za kufanya za kumwingizia kipato?
Mbona kuna wanawake wengi tu wanaojiwezesha wenyewe bila kuwezeshwa?
Huyo Faiza hana akili za kutosha kuweza kujiwezesha mwenyewe?
Ndio tupo wengi tumejiwezesha wenyewe lakini huyu baada ya kuachwa naona ka kajikatia tamaa vile....
* Nakubaliana na wewe, hiyo sababu moja isingetosha...
Basi kama kajikatia na tamaa ni afadhali kwanza anyang'anywe hiyo custody ya mtoto ili aweze kwenda kutafuta msaada wa matatizo yake [pengine ana matatizo ya kiakili]na baada ya hapo afanyiwe tathmini kama karudi kwenye hali ya kawaida ili kuangalia uwezekano wa kurudisha tena haki yake ya uangalizi na ulezi wa mtoto.
Kwa sasa, kulingana na matendo yake kiujumla kama ilivyoonwa na mahakama, hafai kuwa mlezi na mwangalizi wa huyo mtoto.
Hafai kabisa.
Labda baada ya hili anaweza kujifunza akaamua kubadilika kwa ajili ya mwanae..
Akijirekebisha inawezekana akapewa mtoto ili amlee tena??
Nao wananchi wa Mbeya Mjini nao hamnazo, utamchaguaje mwendawazimu kama Sugu anayetembea na kuzaa na hamnazo kama Faiza? Mwanaume mwenye akili sawa sawa hawezi kufuata malaya kama yule. Huu ni wakati wa wana Mbeya kujipima ili Oktoba ikifika muamue mambo ya maana. Tupa mbali sugu na Faiza.