watu kibao
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 466
- 1,663
Ukimuona yupo tulivu, usidanganyike. Ndani kuna moto wa kisiasa unachemka. Saa iko kwenye dakika ya 88 na sasa ni ama zake aingie kama sub abadili matokeo au akubali kusugua benchi "mitano tena".
Jimbo la Mbeya mjini limegawanywa kuwa Uyole na Mbeya jiji
Tulia tayari kavamia jimbo jipya la Uyole,
Jimbo la Mbeya jiji limebaki wazi, lakini kuna nyuki wanazunguka asali. 🍯 na muda unakwenda, saa ya kisiasa haingoji. ⏳ Mbeya Mjini limetulia, lakini si kwa muda mrefu
Wakati Tulia anajipanga Uyole, Mbeya jiji inamsubiri Sugu, ila chama chake kimekataza wanachama kugombea, Hakuna mwanasiasa anaepitia wakati mgumu muda huu kama Sugu.
Si ajabu tukamuona akivua jezi na kuvaa mpya ya Chauma hata CCM
Chadema wamemnyima tiketi, lakini ushawishi wake uko mtaani, si kwenye meza za chama.