Sugu na Jide ni wasanii wasioguswa, ukiwagusa umepotea kimoja, pitia hapa ushuhudie

Refer O-Ten kipindi anafanya bifu la makusudi kwa Afande Sele.....je aliongeza mashabiki au alipunguza?

Avemaria hebu toa mfano unao wagusa Sugu na Jide au utakao jibu maswali yangu!
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada aliitelekeza thread toka Jana!
Hadi sasa nimepitia michango yote sijaona mchango wowote ulio onesha watu waliopotezwa!

Na bahati mbaya wanaosemwa wamepotezwa ndio wanaotamba hadi sasa!

Kilicho nifurahisha baada ya wachangiaji kushindwa kuonesha kwa mifano kuwa Fulani na Fulani wamepotezwa wameamua kutupa historia za muziki za watu wanao dai hawaguswi!

Nimefurahishwa kupata historia za kina Sugu lakini sijashawishika na madai ya watu kupotezwa!
Bado nasubiri!
 

umejua mziki wa kizazi kipya jana wewe,nadhani rudisha mapenzi yako kwa nyimbo ulizo kuwa unashabikia...Jay d kaingia kwenye mifarakano na maadui wake katika kazi ikiwemo clouds na vibaraka wake,pia kwa sugu ndivyo hivyo...Lakini ukirudi nyuma zaidi utagundua hwa ndio wakombozi wa huu mziki ambao leo umewafanya watu kuvuma hata kwanyimbo zisizokuwa na maadili lakini walipo utoa kina Sugu,Jayd,Prof.Jay,Juma Nature,balozi nikugumu mno..sababu hujui unacho kichangia ndoma umeweza kuongea unavyo jiskia bila kuwa natafakuri ya kina
 

Unarudia yale yale
Maudhui ya sredi ni kuonyesha watu waliopotezwa na hawa nguli na si historia zao
 
Unarudia yale yale
Maudhui ya sredi ni kuonyesha watu waliopotezwa na hawa nguli na si historia zao

kuna muda story inaweza badirika nilitaka kuwafahamisha tuu hao wote kuwa unapojaribu kuwa hunt watu flani katika game ya Kizazi kipya utumie tahadhari sana,lazima uwe na fact....
 

Ni wapi umejibu hata swali langu moja? Nimeuliza ni nani kapotezwa? Na ni kivipi wamepotezwa?
Maana hao mlio wasema wamepotezwa bado wana tamba hadi leo mfano FA na Clouds FM bado wana Fanya biashara vyema tuu!

Kama hoja ni mashabiki hata Sugu na Jide hawapendwi na watu wote!

FA hadi sasa bado ana tesa na nyimbo zake zina chaguliwa na kuchezwa kwenye vituo vikubwa nchini burudani kama Clouds FM and East Africa Radio. na hata kwenye show kubwa za burudani hapa nchini kama Kili Tour na Fiesta zote anapata show.

FA amepiga show karibu zote za Kill Tour na mtu kama anapewa show maana yake ana kubalika na kuhitajika!

Sasa utasemaje mtu huyu kapotezwa? Clouds FM bado wana Fanya vyema na wana wateja wengi hata kwenye show Zao ,Sasa utasemaje wamepotezwa?

Hata huyo Chid Benz inaonesha wazi muziki umemshinda kwa sababu zake binafsi wala si kwa sababu ya kukwaruzana na Jide hili liko wazi!

Kwa hapa mnachofanya ni kusimulia historia za kina Sugu na Jide badala ya kuonesha ni nani walimpoteza na ni kivipi?
 

hivi unataka kunambia show ipi hivi karibuni aliopiga FA kama FA zaidi ya kudandi mgongoni kwa Ambwene???sasa unazungumzia fiesta show ambayo lazima apandishwe jukwaani na mabwana zake clouds,kwa ujumla nilitaka kukuweka sawa katika shutumu ulizo jaribu kuwa tupia sugu na Jaydee ndomana comment yangu haikuwa na uhusiano na mada iliokuwepo jukwaani
 

Ungejua unabishana na mtu wa aina gani, wala usingetumia nguvu nyingi hivyo kupoteza muda wako bure. Watu wengine wana politicize kila kitu.
 

Mkuu inaelekea hufatilii kabisa maswala ya burudani! Kwa taarifa tuu kati ya wasanii walio piga show nyingi za Kili ni Mwana FA na Weusi ambao wamepiga show zote!

Unafikiri tunapo Sema Mwanamziki amepata show nyingi usipotaja show kubwa kama Kill na Fiesta umetenda haki?

Mwana FA kapata show nyingi kuliko Ay na amepata sababu ana kubalika!
Hivi ulitaka apate show gani ili kiwe kipimo cha kutopotezwa?
 
Ungejua unabishana na mtu wa aina gani, wala usingetumia nguvu nyingi hivyo kupoteza muda wako bure. Watu wengine wana politicize kila kitu.

Huyu Lawyer jukwaa lake maarufu ni kuleee Jukwaa la Siasa. Nimejichekea kimoyo moyo nilipomwona huku Celebs forum ingawa forums zote ziko open for every one lakini huyu panamfaa zaidi kule kule. Nimeona kuanzia mwanzo mpaka sasa ameshikilia msimamo wa kutaka wamepotezwa vipi wasanii, kivipi, na nani afu hajibiwi na bado hakati tamaa utafikiri tuko mahakamani.
 
Hao wote ni malegend katika mziki wa bongo but hoja yako haina ukweli wowote, wasanii wengi tu wanakuja na kupotea usitake kuniambia kwamba wote waliopotea sababu ni Sugu na Jide, hell nooooo...... Jipange tena!
 
Hao wote ni malegend katika mziki wa bongo but hoja yako haina ukweli wowote, wasanii wengi tu wanakuja na kupotea usitake kuniambia kwamba wote waliopotea sababu ni Sugu na Jide, hell nooooo...... Jipange tena!

Aiseee
 

mkuu nadhani mnashindwa kuelewana lugha na mkuu WA hpo juu nadhani angetumia usemi WA umaarufu wao umeshuka labda kidogo mngeelewana naungana na wewe kusema kwamba hawajapotezwa!Ila umaarufu Wao umeshuka, kupata show kwa msanii mkongwe cyo uzuri Wa nyimbo zake mpya pekee bali ni background na misingi Yao walijiwekea huko nyuma ndyo maana hta sugu akipanda jukwaani akiimba nyimbo zake za miaka ya90 watu wanashangilia
 
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem

kazaliwa 78
 

unaweza kumfananisha mwana FA wa mwaka huu na mwana FA wa miaka mitano iliyopita?
 
unaweza kumfananisha mwana FA wa mwaka huu na mwana FA wa miaka mitano iliyopita?

Hakuna msanii anaye baki pale pale kila mwaka lazima kuwe na mabadiliko!
Labda unijibu unatumia vigezo gani kusema Fulani kapotezwa!
 

Sasa kama hiyo ni hoja basi naomba uniambie mnatumia kigezo gani kusema Fulani kapotezwa na Fulani hajapotezwa?
 
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem
YAANI umeongea point sana si umeona jamaa kala kona alipoona mbibi unataka kumdodea yupo kwa vigoriiiiiiii!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…