Sugu: Wimbo utakaouzidi ‘Freedom’ utapata zawadi ya shilingi milioni 5

Sasa hamasa kwa nani?

Sidhani kama Mesi, Ronaldo, Suarez au Neymar wanahitaji hamasa za kina Figo kufunga mabao.
sasa kwa Tanzania mesi, ronaldo na suarez ni wakina nani mpaka uwapambanishe na sugu
 
Ni msanii anayechipukia kwa kasi.....ila yeye anachanganya music genre zote, bolingo, hiphop, charanga, rege, bongoflavor...you name it.

Bila kusahau singeli!
 
Huu hapa Blue Ft Sugu ya mwaka 2015


Sugu alipofanya utoto wa kuurudia wimbo


Acha nifafanue jambo hapa, maana naona kuna upotoshaji mkubwa kuhusu huu wimbo.
Ukweli ni kwamba huu wimbo ni mali ya Daxo, aliyetengeza beat, chorus na idea ya wimbo wenyewe.
Blue alienda MJ na kuikuta beat ikiwa tayari ishawekwa chorus zote unazozisikia katika ule wimbo.
Akaiomba, akapewa sharti la umiliki wa wimbo na zile chorus zibaki kama zilivyo. Akakubali.
Akaingiza verse yake, lakini kabla hajamaliza akasema kutokana na idea ya wimbo anaomba aimbe na Sugu.
Daxo akafanya mpango akaitwa Sugu naye akaingiza verse yake wimbo ukakamilika.
Blue akatangaza kuutoa huo wimbo katika kipindi cha kukaribia uchaguzi mkuu.
Sasa akina Ruge baada ya kusikia hivyo ndo wakaanza mambo ya kumshauri Blue asiutoe huo wimbo kwa sababu yupo kwenye list ya wasanii wa kampeni za CCM.
Wakamweleza haitapendeza kutoa wimbo aliomba na mtu wa Chadema ambaye ni Sugu.
Blue alihitaji pesa za CCM na uhusiano wake na akina Ruge akakubaliana nao.
Lakini Blue hakutaka kuwaambia chochote akina Daxo akataka aupotezee wimbo kimya kimya.
Lakini kwa kuwa Daxo Chali alikuwa na malengo nao huo wimbo akawa anamsukuma autoe.
Sasa Blue ile kuona kama usumbufu akautoa huo wimbo kwenye Mkito na YouTube kisha akakausha.
Hakuupeleka redio hata moja, kwa maana nyingine aliamua kuua kwa mtindo huo ili kumalizana na Daxo.
Baadaye MJ wakapata taarifa za kilichotokea kwa Blue hadi kufikia kuupotezea wimbo.
Hiyo ilimkera sana Master Jay na akamjulisha Sugu, ndipo Sugu akaomba kwa Daxo aufanyie version yake.
Daxo akamwambia haruhusu tena kufanyiwa audio, akitaka aufanyie video kabisa ili utoke kwa video.
Daxo aliamua hivyo kwa kukwepa kutokea tena ya Blue, coz alijua msanii akiingia gharama ya video hawezi kukubali ngoma ipotee.
Ndio hivyo tangu wakati Wabunge walipokuja Dar kujisajili Sugu akaingiza verse zake na baadaye akafanya video na Hanscana.
Sasa wimbo ulipotoka na kupokewa vizuri, nadhani Blue alitafuta kiki au alitumwa na watu wake akataka kuuharibia.
Lakini wimbo ni mali ya Daxo na ndio maana Blue hakulipia beat na Sugu hakulipia beat.
Wimbo wa Freedom umesajiliwa Cosota kama mali ya Daxo akimshirikisha Sugu na yule binti aliyeimba Chorus.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa mkuu.

Ova
 
Sugu kaiba wimbo acha kutoka povu kumtetea. Ndio maana umebuma.
 

una rekodi ya ya mazungumzo kuthibitisha hayo unayoandika au mkataba wa umiliki wa wimbo kati ya blue na MJ? au unataka tukuamini kwa kuwa wewe umesema?.. yaani tuamini tu kisa mdaku kasema!!
 
Vipi walishamaliza mzozo Na Mr blue ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…