Sukari inafika kilo1 shilingi 2,000/=(elfumbili)!

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
7,375
Reaction score
6,958
Leo nimeenda kununua Sukari dukani nikakuta inauzwa kilo moja shilingi 1,800/= Hii spidi ya kupanda kwake ninaamini miezi mitatu tu ijayo itafika shilingi 2,000/=!!

Jamani hii kasi ya kupanda bei za bidhaa ni kubwa mno, mbona wakubwa hawashtuki? Yaani hili kwao siyo la msingi kama kupokea jezi ya Ronaldo?

Au matatizo haya hayawahusu?
 
vuta subira mkuu, yanapikwa maisha bora kwa kila mtanzania....................
 

Pole san Mzizi wa mbuyu speed hiyo ndo itatumika kuwachaguwa mafisadi wasio kuwa makini/uchungu wa nchi yao. Mungu atusadia watanzania walione hili
 
Nilisoma somewhere (au nilisikia) that sukari sio nzuri sana kwa afya.
I am not very sure.
But these days nimehamia kwenye asali (natural).
May be we should try this.
 
Kuna wakati tulikuwa na thread iliyotaka kujaribu kuweka rekodi za bei za vitu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.

Labda ingefaa kujaribu hiki kitu, kitawapa watu walio mbali picha ya thamani ya shilingi inavyoshuka, bei za vitu zinavyopanda kwa kasi na hata kuweza kulinganisha bei za vitu sehemu mbalimbali za Tanzania.

Tunaweza kuweka bei za vyakula, bidhaa mbalimbali za nyumbani na vifaa vya ujenzi.

Unaweza kuwa umetoka bongo in the eighties unafikiri ukimtumia mtu laki itamfaa sana kumbe inatumika siku mbili tu.
 
Nilisoma somewhere (au nilisikia) that sukari sio nzuri sana kwa afya.
I am not very sure.
But these days nimehamia kwenye asali (natural).
May be we should try this.

Je kwa watoto itakuwaje kama wamezoe hiyo sukari, itakuwa ngumu kuwabadilisha
mm situmii sukari mana chai situmii
 
Ndege ndo kwanza inapaa, wewe unalalamika, hujui engine moja imeleta hitilafu, rubani wetu anatafuta namna ya ku land kwa dharura
 
sukari=tsh 1800
mchele=?
unga(sembe)=?
maharage=?
nyama=?
kuku=?
bei za hizo bidhaa ni sh ngapi sasa hivi?
 
Wakati che nkapa anaondoka madarakani kilo ya sugar ilikuwa 600, maharage 350. mchele 700-800, pakti ya chumvi 100-150, kilo ya unga ilikuwa 400. sasa nadhani tunafahamu wapi tunaelekea
 
Kuna njemba ilikuwa inachekelea thamani ya shilingi kuporomoka kwa kuwa ana account ya dola wenzie wakamng'ong'a akaondoka kikaoni, na ndo dizaini ya watu hao mmewapa dhamana ya kulinda uchumi wa nchi yenu!
 
sukari=tsh 1800
mchele=?
unga(sembe)=?
maharage=?
nyama=?
kuku=?
bei za hizo bidhaa ni sh ngapi sasa hivi?

Per kilo bei ni:


Mchele 1400
Unga 800
Mharage 1300
Nyama 4000
Kuku 7000/8000
 
sukari=tsh 1800
mchele=?
unga(sembe)=?
maharage=?
nyama=?
kuku=?
bei za hizo bidhaa ni sh ngapi sasa hivi?

Mbebabox, na wewe ni walewale wanaoletewa kila kitu nyumbani? maana wenzetu hawajui kabisa bei ya bidhaa. kila kitu wanaletewa na wenye viwanda au maduka
 
 
Per kilo bei ni:


Mchele 1400
Unga 800
Mharage 1300
Nyama 4000
Kuku 7000/8000

kwa namna hii lunch ya wali+kuku ni kama sh 10,000 bila vinywaji/matunda etc
 
Mbebabox, na wewe ni walewale wanaoletewa kila kitu nyumbani? maana wenzetu hawajui kabisa bei ya bidhaa. kila kitu wanaletewa na wenye viwanda au maduka

hapana kaka,hata ukiletewa hadi nyumbani si unalipia na delivery charge,siko tz kwa sasa ndio maana sijui bei za vyakula kwani zinapanda kila mara.
 
Maisha bora kwa kila mdanganyika hayo mkuu. Vumilia tu.

Subiri ngonjera za mafanikio ya awamu ya nne uje uyasikie mwenyewe. Mwezi wa kumi si mbali!

Ajabu ni kwamba hutasikia wadanganyika wakiuliza hilo. Woote wataungana na matajiri na wafanya biashara na uwt kushangilia chama cha ma........ tanzania kudai ushindi wa kishindo.
 

Actually the price should go down, but in reality it is not like that. Ask me why???
It is because of greedy and people's ignorance about money.
 
Dah, jamani kwa kasi hiyo tutakunywa vyenye sukari kweli? Lakini tatizo nini manake tunalima wenyewe kule Mtibwa, Kilombero na Kagera na ningehisi cost of production iko chini sasa kwanini ipande kiasi hicho na haiagizwi nje kwa kiasi kikubwa? Lakini sawa ni mpangwo wa maisha bora kwa kila fisadi na kabwera tutajiju.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…