ndanda masasi
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 772
- 1,177
Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe.Selemani Bungara (Bwege) ametangaza kukihama chama Cha Wananchi Cuf na kuhamia chama cha ACT Wazalendo azalendo mara baada ya bunge kuvunjwa hapo kesho.
---
Ifahamike kuwa, nimeitumikia nafasi ya uwakilishi wa wananchi kwa maana ya ubunge wa Kilwa Kusini kwa vipindi viwili mfululizo kupitia CUF Chama cha wananchi, hivyo sina budi kukishukuru chama changu kwa kunifikisha hapa nilipo na naahidi hapa kuwa sitokisahau kamwe katika maisha yangu yote.
Niliipenda, kuipigania na kuitetea CUF Jimboni kwangu Kilwa Kusini, majimbo mengi ya Kusini na kwingineko Tanzania kwa moyo wangu wote.
Niliipenda sana CUF kwa mapambano yake ya kupigania HAKI SAWA KWA WOTE. Ninasikitika sana kuwa CUF ya sasa imeacha mapambano hayo yaliyoijengea heshima na imani kubwa ya wananchi.
Hivyo basi, ninawatangazia rasmi Watanzania wote kuwa Bunge likimaliza muda wake nitajiunga na ACT Wazalendo.
Nimejiridhisha kuwa ACT Wazalendo ni jahazi sahihi la kupigania demokrasia, haki na maendeleo ya Watanzania.
Suleiman Bungara (Bwege), Mbunge wa Kilwa Kusini.