Suluhisho la matatizo ya ualimu ni kuacha ualimu

LOVED

Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
49
Reaction score
24
Walimu wanalalamika sana juu ya malimbikizo ya mishahara,madai ya fedha za likizo na migomo yao kutokuwa njia mbadala ya kupata haki zao.Mtazamo wangu ni kuwa ili wajikomboe, wote wanaolalamika waache ualimu waingie sekta nyingine.Mf kwa kuongeza elimu yao,au kwenda ktk biashara.Wengi ambao walikuwa walimu wakaacha kazi hiyo wanakiri kuwa na mafanikio kuliko wale ambao walioanza nao kazi.
 
Wendolipumbafu lamwisho kabisa eti wakaongeze elimu zao kwani kila aliye mwalimu anaelimu ndogo?
 
Hv kama wote tukiwa makasisi nani atakae toa sadaka? Hebu jarb kufikiri na kutafakari kidogo endapo wote tungekuwa wafanyabiashara! Tafakari....
 
Hazikutoshi.Una upeo wa kufikiri jinsi ya kwenda haja tu.'Look before you leep'
 
Kwahiyo nawwe unajiita Great thinker kwa ushauri wako kama huo!
 

Hivi uliishia darasa la ngapi vile? Waalimu wakiacha kazi utafundisha wewe? Watu wengine mh... "Bora ukose mali, upate akili". Huyu mleta mada anatambulisha wale wengi waliofika bila ya kujua kwa nini walikwenda shule. Uyu ni miongoni mwa wale wanaoamini kusoma ni kuishia darasa la saba au kidato cha nne. Sijui watu wasipofundishwa wataalamu mbalimbali watazaliwa kutoka angani.
 
mleta mada umeona walimu walivyochachamaa leo unalo ............. usiku mwema lakini
 
Nimeamini utetezi wa mtanzania utatoka mbali ........................... na ninachoamini mleta mada hakuwa na nia mbaya

isipokuwa ametafsiliwa vibayaa
 
Ingawa sikubaliani katika mengi na mtoa mada alosema, ila nadhani imefika mahali Walimu/viongozi wao wasilalamikie tu madai ya malimbikizo yao na madai ya vitu vidogovidogo kama hela za nauli nakadhalika, je hzo bilioni ishirini wanzodai wakilipwa lets say 2moro, je watakuwa na na lakuenda mbele ya media na kusema nini? Nafikiri Walimu wangeangalia kwa upana mkubwa matatizo yao, ambayo mie nadhani haya ni machache kati ya mengi:

1. Mishahara iendane at least na kada nyingine. Mfano mdogo kabisa ni kama huu ambapo Mwl. aliyemaliza chuo kikuu labda kasoma B.ed in arts akiajiriwa katika shule za sekondari huanza na daraja la TGTS D1 wakati mwenzie aliyesoma kozi hiyo hiyo huanza kwa daraja la TGTS E1 ambao wanatofautiana karibia shilingi laki moja.

2. Moja kati ya sifa ya mwalimu kupandishwa daraja ni pamoja na kuongeza kiwango cha elimu. Siku hizi hata usome vipi unabaki katika utaratibu wa kawaida wa kupanda cheo kutokana na mda ulotumika kazini. Mf. Mwl aliyekuwa na diploma mwenye ngazi ya mshahara TGTSC1 akisoma na kupata bachelor ataendelea na mshahara huo huo wakati vijana walio maliza nae bachelor wanakula TGTSD1!

3. Mazingira ya utendaji kazi ni mgumu sana hasa kwa walim walio pembezoni, kuna umuhimu hao kupewa upendeleo maalum mfn wakiamua kujiendeleza serekari ighalimie masomo yao

4. Unaweza kuongezea na za kwako!
 
1.Unapanda daraja leo,unaanza kulipwa baada ya miezi 5,na malimbikizo utalipwa baada ya mwaka!
2.hakuna posho,teaching allowance
 
mi nakubaliana na mtoa mada!endapo walimu wengi watachange proffesional zao na kwenda kwingine serikali itafungua masikio na kurekebisha hali iliopo ili kumaintaini walim waliobaki.so matatizo yote yataisha.
 
Nimeamini utetezi wa
mtanzania utatoka mbali ........................... na ninachoamini
mleta mada hakuwa na nia mbaya

isipokuwa ametafsiliwa vibayaa

uko sahihi walimu wamemtafsiri vibaya mtoa mada.
 
kusingekuwa na BAN ningeporomosha matusi!!!!!namwachia Mungu!
 
Kama ndoa yako imejaa matatizo unaweza kufanya yafuatayo: 'piga chini ndoa nenda kaanzishe mausiano mengine au kaa kimya na jifanye hakuna tatizo'- By Fina Mango.

Muanzisha mada huko sahihi haya malalamiko na kufanya kazi chini ya kiwango kwa walimu sio tiba ya matatizo yao.
 
nafikiri alimaanisha asomee kitu kingine,kwa mfano kama ana B.A.,Ed.ansomee M.A DS,kwa mfano tu

Wendolipumbafu lamwisho kabisa eti wakaongeze elimu zao kwani kila aliye mwalimu anaelimu ndogo?
 
Wendolipumbafu lamwisho kabisa eti wakaongeze elimu zao kwani kila aliye mwalimu anaelimu ndogo?

asante kwa werevu wako.Ila ukumbuke ukiwa umebarikiwa hekima basi jua wapo wapumbavu kama mimi.But thanks
 
Hv kama wote tukiwa makasisi nani atakae toa sadaka? Hebu jarb kufikiri na kutafakari kidogo endapo wote tungekuwa wafanyabiashara! Tafakari....

Wahanga wa field hii wanaelewa nachozungumzia ingawa nashukuru kwa kunipa muda wa tafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…