tuacheni nidhamu ya woga Wananchi. Hii n nchi yetu, watu wachache hawawezi kuiendesha watakavyo kama wanavyoendesha familia zao..we must b strong and present our DEMANDS..and not requests, lazima tuhoji kwa umoja na ni LAZIMA watoe UFUMBUZI na siyo majibu ya kisiasa...wao walisoma kwa mikopo, na im sure hawakumbuki hata kuilipa..kwa nn cc tunazungushwa utafkiri wanatupa bure! Watanzania wenzangu, huu c muda wa kutegeana, tusiishi kwa mazoea, nyakati zimebadilika...ukitazama vizuri, utagundua kuwa tunaishi kweli, lakini haya c maisha ambayo tunapaswa kuishi...elimu(ya kata) tunayoipata , mikopo tunayoikosa, ni vikwazo vikubwa katika maisha, na hasa tukizngatia kuwa tupo kwenye soko la ushindani wa kielimu, soko la Afrika mashariki na dunia nzma kwa ujumla..Watanzania, tutachomoka kweli kwa staili hii??..wapo watakaotoka, lakini wengi tutabaki...tusikae kimya tukiogopa kwa kutishiwa FFU, Wakat FFU hao hao n wenzetu, ndugu zao pia wamekosa mikopo, na maisha yao magumu pia. ni FFU yupi unayemfahamu anamiliki VX V8? lakini n maofisa wa ngapi wa bodi wanamiliki zaidi ya hapo! hatusemi kama n wezi, hatuna ushahidi..lakini tunautafuta..ila wawe na ile hali ya kutujali wanafuzi ambao tunadamkia offisini kwao na tunazungushwa ..tusiwe na wasiwasi FFU watakuwa pamoja nasi kama tutadai madai yetu kwa utaratibu na hasahasa madai hayo yakiwa YAMSINGI...Tunaimba MUNGU IBARIKI TANZANIA..lakini hizo baraka zitakuja vp kama tunayafumbia macho maovu yanayojitokeza kwa sababu ya hofu ya kuwekwa 'ndani'? tutabarikiwa sote tukiwa nchi moja kama sote tutakuwa pamoja katika kutafuta haki tukifuata Taratibu na kwa kuzingatia Kuwa sheria n msumeno usiowakata wanyonge tu, bali hata mabepari wanaitumia mihuri ya offisi zao katika kuonea wanyonge, na kujitengezea sheria zinazowakinga dhidi ya adhabu...