Grand Canyon
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 545
- 1,191
Jiji la Mwanza lina changamoto ya msongamano wa magari kwa sababu barabara inayounganisha Mwanza na Tanzania ina njia mbili tu. Hiyo ni barabara ya Kenyatta. Barabara inayounganisha Mwanza na njia ya Kenya ina njia 3.Ni barabara ya Nyerere.
nini kifanyike?
Magari ya Abiria yasiingie katikati ya mji. Ichongwe barabara kutokea Pepsi itakayopita Igogo hadi Bugarika(Bugando) kisha Ishukie Mabatini.Mlima wa Mabatini kwenda Bugarika utakwanguliwa kidogo sehemu isiyo na mwinuko mkali linapopita bomba la maji kisha lijengwe daraja ili kupunguza mpando(Ona picha).
Kituo cha mwisho kuingia mjini kutoka Kisesa kitakuwa Mabatini kisha magari yanayokwenda Buhongwa yanapita Bugarika yanateremka hadi Pepsi kupitia Igogo.
Kisha ichongwe barabara nyingine kutokea Mabatini kupitia Isamilo hadi daraja la Rock City mall. Hiyo itakuwa barabara ya Airport-Isamilo-Mabatini-Kisesa, au Airport-Mabatini-Igogo-Nyashishi, au Nyashishi-Igogo-Mabatini-Kisesa.(ona picha)
Isamilo,Mabatini,Bugarika, na Igogo(Pepsi) kuwe na vituo vya daladala.Wateja watakuwa wanashushwa kwenye hivyo vituo. Kwa hiyo Wamachinga watakimbia jiji kwenda Mabatini,Isamilo,Bugarika,Pepsi ili kufata wateja.