SoC04 Suluhisho la tatizo la upungufu wa ajira nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

evergreen juggle

New Member
Joined
May 28, 2024
Posts
2
Reaction score
3
Muda mrefu sasa mfumo wetu wa elimu umekuwa hauendani na mahitaji ya soko la ajira, lakini pia hauendi sambamba na mabadiliko ya dunia katika nyanja ya teknolojia yaliyopo kwa ujumla kwani kama taifa tumekuwa nyuma zaidi huku baadhi ya mataifa yakituacha mbali sana katika nyanja ya elimu hususani elimu inayo husanisha kipaji cha mwanafunzi pamoja na utolewaji wa elimu ya ufundi na mafunzo stadi.

Idadi ya watu nchini tanzania inaongezeka kwa kasi sana kila kuchapo.
Uhitaji wa vijana wahitimu katika soko la ajira kwa maana ya ajira mpya hauendani na idadi ya wahitimu wanaopatikana kwa mwaka, pia hata idada ya wastaafu kwa mwaka haishabiani kabisa na wahitimu waliopo kwa mwaka husika.

Ongezeko hili la watu nchini linaenda sambamba na ongezeko la changamoto ya ukosefu wa ajira kwa watanzania, ajira katika makundi yote kwa maana ya waliosoma na ambao hawajafanikiwa kusoma na kupata maarifa. Kwa lugha rahisi na yakueleweka tunasema ajira zilizopo katika sekta zote kwa maana ya sekta binafsi na serikalini hazitoshelezi.

Kwa miaka ya hivi karibu hasa baada ya kuanzishwa kwa shule za sekondari za kata,kumekuwa na ongezeko kubwa sana la idadi ya wanafunzi wanao faulu masomo yao kisha kuendelea na elimu katika ngazi tofauti tofauti ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya uanzishwaji wa shule hizi.Bila shaka malengo ya serikali katika mradi huu yametimia, na kwa dhati kabisa nitoe pongezi kwa waliobuni mradi huu kwa manufaa ya wananchi wa uchumi wa chini.

Idada kubwa ya vijana wahitimu kuanzia ngazi ya shule ya msingi,sekondari,vyuo vya Kati na vyuo vikuu walio na viwango vya elimu kuanzia cheti, diploma, shahada na astashahada,walio wengi hawanufaiki wala hawainufaishi Jamii zao kwa elimu waliyopata kwani elimu waliyopata baada ya mapambano ya muda mrefu wawapo shuleni haijawajenga katika misingi ya kujiajiri na kujiamini katika soko la ajira,badala yake imejikita zaidi katika misingi ya kuajiriwa na kuendelea kuwa tegemezi badala ya kuwa chachu na suluhu ya changamoto zinazoikabiri Jamii.

Ukiondoa dhana ya elimu kama nyenzo ya kumkomboa na kumkwamua binadamu kutoka katika ujinga kwa kujua kusoma na kuandika hii haiondoi ukweli kuwa elimu ndiyo nyenzo thabiti na yakinifu katika taifa na Jamii yetu katika kuyafikia maendeleo yetu, kwa maana ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Hivyo kwa kuzingatia msingi wa elimu kama nyenzo ya ujuzi na maendeleo,kama Taifa hatuna budi kubadili mfumo wetu wa elimu ili kutoka hapa tulipo ambapo ni kwenye mkwamo na kwenda hatua bora zaidi yenye mafanikio. Kwani hapa tulipo sasa hatuna tofauti na timu ya mpira wa miguu inayotumia mabeki kufanya jukumu la kufunga kisha viungo na washambuliaji wafanye jukumu la kukaba huku timu ikitarajia ushindi wa kishindo ulioambatana na magoli mengi!,ni ngumu.

UBORESHAJI: Ili kuondokana na changamoto ya wimbi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira nchini,Uboreshaji unapaswa kufanyika katika ngazi tatu za utoaji elimu. Katika ngazi hizi serikalini ianzishe mpango maalum wa utoaji elimu uliojikita kati MAFUNZO YA UFUNDI STADI.

  • Ngazi ya shule za msingi(V-VI).​
  • Ngazi ya shule za sekondari (I-VI)​
  •    Ngazi ya vyuo vya ufundi​
NGAZI YA SHULE ZA MZINGI (V-VI)
Katika kujifunza, tafiti na makala mbalimbali zimeonesha kuwa ni rahisi sana mtoto kufundishwa,kujifunza na kuelewa zaidi kile alichofundishwa akiwa katika umri mdogo. Mataifa ya wenzetu walioendelea hutumia sana mbinu hii katika kuhakikisha wanawajenga vijana wao wakingali wadogo na kuwafanya kuwa na uwezo mkubwa. Katika ngazi hii wanafunzi kuanzia darasa la tano hadi sita waanze kupewa mafunzo ya awali ya elimu ya ufundi na mafuzo stadi ambayo yatahusisha fani na juzi mbalimbali ambazo ni chachu ya maendeleo lakini pia zile zenye kuhitajika katika soko. Mafunzo haya ya awali yafanane kabisa na mafunzo ambayo hutolewa na taasisi mbalimbali za mafunzo ya ufundi na stadi mbalimbali. Katika ngazi hii mafunzo yajikite zaidi katika kumjengea mwanafunzi msingi wa awali.
Mafunzo haya stadi kupitia mpango maalum yataweza kumjenga mtoto hivyo kumuwezesha kuwa na ujuzi wa awali wa fani husika inayohusu maendeleo na mabadiliko mahususi ya teknolojia.

NGAZI YA SHULE ZA SEKONDARI,(I-VI).

Baada ya kuhitimu shule ya msingi na wanafunzi kufanikiwa kupata mafunzo ya awali. Katika ngazi hii wanafunzi waanze kupewa mafunzo yaliyoboreshwa zaidi kutoka katika kujikita kwenye matumizi ya maelezo hadi katika matumizi ya vitendo na nyenzo. Mafuzo yapande na kuendelea kuboreshwa zaidi kutoka darasa moja hadi jingine, mfano katika ngazi hii mwanafunzi afundishwe fani husika kwa kutumia kifaa husika.
Muhimu: mpango huu maalum, hasa katika ngazi hii itahitaji mchango na uangalizi wa karibu wa mzazi katika kuhakikisha anaimarisha ujuzi wa mwanafunzi. Katika kipindi cha rikizo na siku za mapumziko za mwisho wa juma, muda huu utumike kumpeleka mwanafunzi katika vituo mbalimbali vinavyofanya shughuli zinazoendana na mafunzo (fani) anayojifunza mwanafunzi.
mafunzo haya stadi yatengewe muda wake kuondoa kuingiliana na muda wa vipindi vya masomo ya kawaida. Lakini pia vipindi hivi vitiliwe mkazo na msisitizo kama ilivyo kwa masomo mengine.
NGAZI YA VYUO VYA UFUNDI NA MAFUNZO STUDI

Katika ngazi hii mafuzo yaboreshwe kwa kuhakikisha vifaa vinavyotumika kufundishia wanafunzi viwe ni vile vilivyo bora vinavyoendana na teknolojia ya sasa.
Mwanafunzi atajifunza kwa vitendo na uhalisia zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo mwanafunzi huanza ngazi ya awali iliyojikita katika maelezo kisha baadae vitendo.
Kwa vile mwanafunzi alishaanza kusoma fani husika kutoka ngazi ya awali(shule ya msingi), hadi anahitimisha mafunzo yake katika ngazi hii itamfanya kuwa mbobezi na mwenye maarifa makubwa zaidi katika taaluma ya stadi husika na kupelekea kujiamini mbele ya majukumu yake.

MATOKEO YA UBORESHAJI WA ELIMU.

  • Ajira; kijana ataweza kujiajiri mwenyewe kwa kufanya kazi mbalimbali zinazoendana na taaluma yake kwani kazi nyingi za ufundi stadi huhitaji mtaji mdogo kuanzishwa ukilinganisha na kazi za taaluma ya masomo mengine. Hii itapunguza kama si kuondoa kabisa changamoto ya ajira kwa vijana​
  • Ujuzi; kijana wa kitanzania atafanikiwa kuhitimu masomo yake yakienda sambamba na kupata ujuzi wa fani husika katika umri mdogo,na kumfanya kuwa na sifa ya ufundi mwenye stadi kubwa katika taaluma husika​
  • Utegemezi; idadi kubwa ya vijana ambao ni tegemezi, mbali na kuwa na elimu ya juu lakini hawana ujuzi unaohusanishwa na fani za ufundi litapungua.​
  • Uharifu; itapunguza matendo mabaya ya uharifu kwani makundi mengi ya uharifu yanavinasaba na uwepo wa kundi kubwa la vijana ambao hawana shughuli ya kufanya kupata kipato Ili kukidhi mahitajai yao.​
  • Maendeleo ya haraka; kama Taifa na mtu mmoja mmoja katika Jamii maendeleo yataongezeka kwani nguvu kazi ya taifa itaimarika na kuchochea maendeleo.​
 
Upvote 5

Hakika ni mafanikio makubwa, ile suala la amefaulu lakini kakosa nafasi ilikiwa sio njema kabisa. Ilijenga kama hali ya waliokosa kuwaonea wivu waliopata maana wameziba nafasi zao.

Katika kujifunza, tafiti na makala mbalimbali zimeonesha kuwa ni rahisi sana mtoto kufundishwa,kujifunza na kuelewa zaidi kile alichofundishwa akiwa katika umri mdogo. Mataifa ya wenzetu walioendelea hutumia sana mbinu hii katika kuhakikisha wanawajenga vijana wao wakingali wadogo na kuwafanya kuwa na uwezo mkubwa
Kuukuza na kuutunza udadisi wao muhimu
 
🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom