SoC04 Suluhisho la upatikanaji wa bidhaa za afya vituoni hususani bidhaa za dawa

SoC04 Suluhisho la upatikanaji wa bidhaa za afya vituoni hususani bidhaa za dawa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Dino ngalowoka

New Member
Joined
May 19, 2024
Posts
1
Reaction score
0
UTANGULIZI.
Licha ya selikari kufanya jitihada kubwa katika huduma za afya, ikiwemo majengo ya kutolea huduma za afya na wataalamu mbalimbali. Bado Kuna changamoto katika upatikanaji wa bidhaa za afya hasa bidhaa za dawa.

Wizara ya afya kupitia bohari ya dawa (MSD) imekuwa ikipeleka dawa, vitendanishi vya maabara, na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma, na visivyo vya umma Kila baada ya miezi miwili na Kila panapohitajika.

Lakini bado kumekuwa na changamoto ya uwepo wa bidhaa za afya za uhakika katika vituo husika. Hasa vituo vya umma.

MAPENDEKEZO
1. BOHARI YA DAWA (MSD) IANZISHE VIWANDA VYA DAWA KATIKA KANDA ZAKE.

Hapo awali bohari ya dawa ilikuwa na majukumu matatu ambayo ni 1.manunuzi, 2.uhifadhi na 3. usambazaji wa bidhaa za afya kwa vituo vilivyokubalika. Baadae ikaongezewa jukumu jingine 4. Uzalishaji wa bidhaa za afya. Moja ya kiwanda Cha MSD kipo makambako na kinajihusisha na uzalishaji wa mipira ya mikono (gloves)

UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU.(Miaka 5-15)
-Maghara ya kuhifadhia bidhaa za afya, yaliyopo Kila Kanda yangeweza kutumika kama viwanda vya dawa mbalimbali, kulingana na aina ya magonjwa yaliyopo katika ukanda husika.

- Maghara na ofisi za bohari ya dawa yangetumika katika hatua ya mkoa na wilaya. Kwa maana Kila mkoa uwe na bohari kuu ya dawa kwa mkoa mzima, pia Kila wilaya iwe na bohari yake pia kwa ajili ya wilaya husika.

UFANISI
1. Tutapunguza tatizo la ajira , kwa kuajili wataalamu mbalimbali katika nchi.
2. Tutaongeza Ufanisi kwa wataalamu wetu.
3. Tutapunguza gharama kwa selikari, fedha zinazotumika kuagiza dawa nchi za nje.
4. Tutapunguza hasara ya bidhaa za afya kufa (expire)katika baadhi ya bohari zetu.

2. UBORESHAJI WA STOO ZA KUHIFADHI DAWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
Kwa sehemu kubwa, upande wa vituoni hakuna stoo ambazo zilijengwa tangu awali kwa lengo la kuhifadhia bidhaa za afya. kwa sehemu kubwa chumba Fulani hutengwa na kufanyika kama ndio stoo.
Hii hupelekea kuwa na kuagiza bidhaa kwa uchache kulingana na ukubwa wa stoo na sio kulingana na matumizi au mahitaji ya wagonjwa.

UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU (miaka5-15)
1. Selikari ihakikishe kuwa stoo zinajengwa Kila kituo kulingana na mahitaji husika.
2. Usimamizi wa STOO uwe chini ya wataalamu wa dawa kuanzia ngazi ya zahanati.
3. KUANZISHA VITENGO VYA UTENGENEZAJI WA DAWA (COMPOUNDING UNIT)KATIKA KILA HOSPITALI, KWA KUANZIA NGAZI YA HOSPITAL YA WILAYA

  • Vitengo hivi vitasaidia sana upatikanaji wa baadhi ya dawa ambazo kutokana na sababu mbalimbali zinaweza zisipatikane sokoni.
  • wafamasia wanao uwezo wa kutengeneza na kuchanganya viambata mbalimbali ili kuleta dawa inayoweza kumsaidia mgonjwa.
UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU (Miaka 5- 15)
- liwe ni takwa la kisheria Kila hospital iwe na compounding unit inayofanya kazi.
4. KUBORESHA MIFUMO YA MNYORORO WA UGAVI.(Mwaka 1)
Hususani katika kuzuia bidhaa za afya ku - expire
Kuongeza msukumo wa Utoaji wa taarifa kati ya wateja wa bohari ya dawa (vituoni) na watendaji wa MSD hasa pale kunapokuwa na dawa ambazo hazijanunuliwa kwa kipindi kirefu.
Taarifa zitolewe kwa wafamasia wa mkoa na wilaya ili niweze kuwafikia watendaji wao.

MWISHO
Hii ndio Tanzania niitakayo, ambayo ninaamini yakifanyika hayo tutaongeza wigo wa upatikanaji bidhaa za afya vituoni mwetu na kujenga Tanzania yenye watu wenye afya Bora.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom