SoC01 Suluhisho la upotoshwaji wa taarifa mitandaoni na udukuzi nchini tanzania

SoC01 Suluhisho la upotoshwaji wa taarifa mitandaoni na udukuzi nchini tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

GUAVA TECHNOLOGIES

New Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "stories of change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litalenga zaidi kuzuia UPOTOSHWAJI WA TAARIFA MITANDAONI na UDUKUZI katika Nchi yetu ya Tanzania.

Nitazungumzia mambo yafuatayo:

  • Nini chanzo cha upotoshwaji wa taarifa mitandaoni na Udukuzi?
  • Nini Kifanyike kwa nchi yetu katika ukuaji wa Teknolojia?
  • Suluhisho litaleta Mabadiliko gani kwa nchi yetu?
Fuatana Nami hatua kwa hatua:

NINI CHANZO CHA UPOTOSHWAJI WA TAARIFA MITANDAONI NA UDUKUZI?

Chanzo kikubwa kinacho sababisha kuwako na Kuzuka kwa taarifa zisizo rasmi ni UKOSEFU WA AJIRA watu wengi hususani vijana wameamua kutafuta kipato kwa kujihusisha na mambo haya kwani wakiamini ni njia moja wapo ya kujikwamua kiuchumi. Ambacho anaweza kuwako tu na kifaa chake cha ki-electronic na kufanya kile ambacho anaona yeye ni sahihi lakini sivyo.

NINI KIFANYIKE KWA NCHI YETU KUZUIA UPOTOSHWAJI NA UDUKUZI KATIKA UKUAJI WA TEKNOLOJIA?

Tazama mfano huu:

Kama nchi yetu ya Tanzania tuliweza kuzuia upotoshwaji wa taarifa kipindi cha uchaguzi, Je? Tunashindwaje kuzuia moja kwa moja kuzuia hili kwa watu (Watanzania) Kujijengea self discipline?

TAZAMA SURUHISHO HAPA:

Sera ya kutumia Namba za NIDA ili kuweza kupata mtandao.


Asilimia kubwa ya watu wanaofanya hivi ni watu wazima miaka 18 na kuendelea ambao wote wapo kwenye mfumo mzima wa Utambulisho wa Taifa.

Nini kifanyike?

Kuwe na Usajili wa matumizi ya kimtandao Kama TAIFA ambao kila mtanzania atalazimika kujisajili kwa kuweka namba yake ya NIDA. Na mtanzania yeyote ambaye hataweza kujisajili hatoweza kupata/kutumia mtandao iwe ni Whatsapp, Twiter, Facebook, Instagram, Youtube, Linkdin, na nk.

Nini kizingatiwe?

Katika matumizi haya Namba ya NIDA itaonyesha A-Z taarifa za mtumiaji wa mtandao na si vinginevyo, hivyo kama atakiuka sheria za matumizi ya kimtandao atachukuliwa hatua.

Pia katika mfumo huu ni lazima kuwe na content filter(Kipima Maudhui) pindi mtumiaji wa mtandao anataka kutuma kwa umma.

“”Hakika Inawezekena🙏””

  • Kufungua MAABARA ya kuwaendeleza Vijana wanajihusisha na masuala ya TEHAMA pindi wamalizapo masomo yao vyuoni na pia kufanyika kama kituo cha Makampuni, Watu binafsi na serikali kwa ujumla kupata wataalamu watakao weza kuwasaidia katika vituo vyao vya kazi.
  • Kuwavuta vijana kuhudhuria semina Mbali mbali za ujasilia mali hivyo waweze kutumia teknolojia katika kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumii kwa elimu waliyo ipata na teknolojia walionayo nasi kupotosha umma na kusababisha udukuzi.
  • Kuwapatia elimu watanzania wote kuhusu vitu gani vinavyo weza kuwa hatarishi kwao kwa kuweza kudukuliwa.


SULUHISHO LITALETA MABADILIKO GANI KATIKA NCHI?

  • Itaongeza nidhamu katika matumizi ya mtandao kwani kila anachokifanya anajulikana ni nani kafanya annatoka wapi, kazaliwa wapi, mawasiliano yake na n.k
  • Kuibuka kwa fursa mpya kwa watu wa Tehama kwani watajaribu kutafuta njia mbadala wa kujipati kipato na kuachana na kupotosha umma na kufanya udukuzi.
  • Kupitia maabara tutaweza kuwaweka Pamoja vijana wanaojihusisha na Tehama kwani tutaweza kuvumbua mambo mengi makubwa yatakayoweza kuilinda nchi yetu katika masuala mazima ya udukuzi na kupotoshwa kwa taarifa.

TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU.

Usisahau ku vote, Ahsante…
 
Upvote 1
Back
Top Bottom