Suluhisho: Tatizo la mita ya luku kugoma kupokea token

Hapo namba 3 nifafanulie mkuu...umeme hamna kabisa umezima luku imeisha je nichomeke tu? Ila betri zinafanyakazi ni mpya...
Yes chomeka ndugu. Hiyo remote siyo kama ya tv, pole sana.
 
Nimefuata hivyo ulivyoelekeza namba zinaingia ina search lakini inaonyesha error..labda nijue hii kitu he hata kama nimeweka betri na zinafanya Kazi he kuna haja tena ya kuchomeka kwenye soketi? Maana umeme umekatika kabisa niko gizani totoro..

-Nasisitiza, ili mita iliyopo kwenye nguzo iweze kuonana na (kiwasilianishi) kwa lugha nyepesi call it remote, hakikisha imepachikwa ktk socket.
- Jambo jingine Nakushauri badilisha Betri ( weka betri mpya) kisha fuata maelekezo niliyo kupa.
- Kama umeme umekwisha kabisa ktk mita yako, nenda kwa jirani yako ambaye ana umeme ukiwa na (kiwasilianishi) remote yako hakikisha anatumia phase unayo tumia wewe (same phase) na pachika ktk socket na iwashe. Ikiwaka ingiza umeme (tarakimu ishirini) na kubonyeza mshale wa enter.
Mita nyumbani kwako ita waka.
- Ikishindikana nitumie namba yako ya simu nikuelekeze.
 

Mkuu hapo bold.... kwa malaymen kama sisi hatujakuelewa. Unamaanisha kama anatumia single phase hawezi kupata umeme kama jirani anatumia three phase?
 
wala vumbi noma sana, yaani hadi mnawekewa mita juu kwenye nguzo!, ni tusi hilo.
Sijui kwanini TANESCO wameamua kufanya hivi. Tulioweka umeme zamani mita bado ziko ndani ya nyumba
 
Mkuu hapo bold.... kwa malaymen kama sisi hatujakuelewa. Unamaanisha kama anatumia single phase hawezi kupata umeme kama jirani anatumia three phase?
anamaanisha line moja
mfn ishawai tokea shoti ukashangaa nyumba ya jilani kutoka nyumba yko umeme upo ila kwako na nyumba ya nne kutoka kwako ndo amna umeme sasa hapo ndo phase moja a.k.a line moja
ikatokea umeme ukaisha wote na betry ya remonte ipo down araf ukienda kwa jilani anaekufuatia kuingiza token inaweza umeme usiwake 7bu si line moja mpka hiyo nyumba ya nne ndo uhakika kuwaka 7bu wote mpo line (phase) moja
 
Mkuu nakushukuru kwa ufafanuzi murua.
 
Nawashukuru sana wote mliochangia kunisaidia..nimefanikiwa muda huu nimetumia sana maelekezo ya Kichoi na saaMbovu , mwisho kabisa nimechomeka kwenye soketi japo umeme haupo ..hapo ndipo iliposoma na token zimekubali...lakini napatwa na maswali kibao INA maana Tanesco hiki kitu hawakijui walishindwaje kunielekeza!!!!!!!!!...asante JF humu kila kitu aisee
 
Sijui kwanini TANESCO wameamua kufanya hivi. Tulioweka umeme zamani mita bado ziko ndani ya nyumba
Mkuu mita za zamani na hizi kuna tofauti kubwa sana.
1. Mita za zamani ni mpaka msoma mita aje na mteja apigiwe hesabu ili kujua bill yake wakati za sasa ni prepaid.
2. Mita za sasa zimeongeza mapato na kupunguza madeni kwakua mita za zamani baadhi ya wateja walikuwa hawalipi kwa wakati.
3. Mita za sasa zinapunguza idadi ya wafanyakazi kwakua hakuna haja ya kuwa na msoma mita kwahiyo kuongeza kipato kwa shirika tofauti na za zamani
4. Faida kubwa ya mita za sasa ni kuwa zinahisi hitilafu (short) ya umeme kwa haraka sana na zina fungua relay ili kutoa umeme na kuepusha nyumba kuwaka moto. Hii pia hutokea pale fundi aliyefanya wiring akikosea kidogo au kuna sehemu ina lose connection basi meter inagoma kabisa kwakuwa ina sense short wakati mita ya zamani haiwezi kufanya yote hayo.
5. Hizi mita za sasa unapotaka kuiba umeme kupitia kwenye mita ni vigumu sana kwakua kuna cover ambalo lazima utoe la ukilitoa hilo automatic kuna button unakuwa ume open so mita inahisi umeme unaibiwa kwahiyo basi inakuwa kwenye 'tempering mode' na huwezi kutoa mpaka uwaone wahusika wakati mita za zamani hazifanyi hivyo.

Note: Hapo namba 4 unaweza ukawa na tatizo mita ikazima kuokoa nyumba yako lakini kwa kutokuelewa unaanza kuwalaumu au kuwatukana tanesco kumbe ulitakiwa kuwashukuru. Hata hivyo tanesco wanatakiwa watoe elimu ya kutosha hasa kupitia vipeperushi kwakuwa ana kwa ana inakuwa vigumu mara nyingi wakati wanaenda kufunga mita huwakuta watoto tu.
Hata wakiviacha vipeperushi bado sisi watanzania ni wavivu kusoma hata ukurasa mmoja tu. Muhimu ni kufuatilia kipindi cha TANESCO na maendeleo binafsi nimejifunza mengi sana.
 
Pamoja sana. Uyashike hayo maelezo kwa ajili ya siku nyingine.
 
Mkuu mi nazungumzia Luku za zamani ambazo pia msoma mita haji kusoma. Mi ya kwangu iko ndani na wala situmii hiyo "remote" naingiza token moja kwa moja kwenye mita.

Hii luku ya sasa (kwenye nyumba nyingime) ndo wameiweka nje na nimepewa hiko kirimoti. Sasa hoja yangu ilikuwa kwa hizi mita za luku... kwanini hii ya sasa wanaifunga nje wakati ya zamani ilikuwa inawekwa ndani ya nyumba?
 
Duh asante kwa somo Zuri
 
Kudhibiti wateja ambao sio waaminifu yaani wezi wa umeme ambao wanachezea mita. TANESCO lazima watakuwa na wasiwasi na mita yako iliyo ndani ya nyumba, labda haiko salama!
 
Kudhibiti wateja ambao sio waaminifu yaani wezi wa umeme ambao wanachezea mita. TANESCO lazima watakuwa na wasiwasi na mita yako iliyo ndani ya nyumba, labda haiko salama!
Lakini ni wao wenyewe ndo waliiweka ndani muzee...
 
...Hiyo ndio meter yenyewe, sio remote hiyo!
Sio kweli mkuu mita ndio ile kwenye nguzo hicho kidude kinaitwa "customer interface unit" (CIU). Kinaweka mawasiliano kati ya mteja na mita kwa kuwa mita yenyewe haina dispay yoyote wala keypad kwa ajili ya kuinteract nayo na kungiza token.
 
Sio kweli mkuu mita ndio ile kwenye nguzo hicho kidude kinaitwa "customer interface unit" (CIU). Kinaweka mawasiliano kati ya mteja na mita kwa kuwa mita yenyewe haina dispay yoyote wala keypad kwa ajili ya kuinteract nayo na kungiza token.
...Nakubaliana nawe. Hiyo inaitwa User Interface Unit. Sasa, hiyo na ile kwenye nguzo si ndio mita yenyewe, au?
 
imejibu reject 2
 
inhemeter yangu. Kila njia hapo juu nimetumia lakini sijafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…