Suluhu kwenye kodi ya kizalendo

Suluhu kwenye kodi ya kizalendo

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Kimtazamo, kodi hii ni muhimu lakini haitekelezeki. Kodi hii huwezi kuita progressive maana imegusa maisha ya wananchi ambao hata basic needs ni shida. Yaani lower end zile charges ni exorbitant.

Nini kifanyike;
Tozo zitoe nafuu mpaka 50k TZS na kwenye miamala ya juu yake ziwe ndogo ili ku discourage watu kutuma miamala mingi ya 50k.
Bunge ni la wananchi. Liitishwe hata kama ni remotely ili kikwazo cha kisheria kama kipo kiondoke.

Kujenga imani ya Serikali, Waziri mwenye dhamana ya Fedha atupishe kwa kuleta sheria ya hovyo na kuwakejeli Watanzania.
 
Upande mmoja mtu anasema tunaongeza pesa kwenye mzunguko, upande mwingine anataka kuzitoa kwa kasi.
Wanatuambia uchumi umeshuka, then wanakuja na negative approach za kudumaza ajira na ukuaji uchumi.
 
Ninamwelewa prof. Assad aliposema 60% ya viongozi wetu hawana uwezo...nadhani ni 80% sio 60% - 70% kama alivyosems
 
Ninamwelewa prof. Assad aliposema 60% ya viongozi wetu hawana uwezo...nadhani ni 80% sio 60% - 70% kama alivyosems
Intellectual arrogance of this time is unparalleled. Jamaa hafai kuwa mwanasiasa, amuulize Mwakyembe
 
Upande mmoja wanasema benki zipunguze charges, ila serikali inafanya kinyume chake
 
Kodi ya kizalendo ila hao wanaojiita wazalendo namba moja(viongozi wa ccm) hawakatwi kodi kwenye mishahara yao, watoto wao wanasoma shule binafsi na za gharama kubwa kama Feza.
 
Kodi ya kizalendo ila hao wanaojiita wazalendo namba moja(viongozi wa ccm) hawakatwi kodi kwenye mishahara yao, watoto wao wanasoma shule binafsi na za gharama kubwa kama Feza.
Kinachosumbua zaidi ni kuunda tume ya kupitia bei. Huu ni ujanja wa ku-assess market situation. Tusipokuwa makini wataendelea. Ina maana km kuna sheria mbaya na haitekelezeki ni lazima iendelee kuwepo au kutumika. Tuliona serikali ya awamu ya tano ambayo hii iliyopo ni proxy yake ikisitisha mengi tu na hata yaliyopo kwenye katiba. Tukubali tunalo la kufanya wakati tume ikiendelea na kazi yake.
 
Back
Top Bottom