ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
HISTORIA FUPI YA MSANII SUMA " G" A.K .A SILAHA MANENO KIPAJI HALISI KUTOKA USWAHILINI...
Kiukweli mimi kama "suma G" katika industry ya Muziki wa Bongo fleva wimbo wangu wa kwanza kunitambulisha kwenye ramani ya Muziki wa Bongo fleva, wimbo huo ulikuwa unajulikana kwa jina la " vidonge vyao" .. pia nakumbuka
Enzi hizo " hot pot family " ilikuwa kama ni familia yetu ya mtaani , " hot pot family" ilikuwa haijihusishi na muziki moja Kwa moja , ilikuwa inahusisha sisi vijana ambao tulikuwa Tunaishi Eneo moja maarufu kwa wakati ule linaitwa "karakata" kule uwanja wa ndege kwahiyo umoja wetu sisi kama vijana wenye vipaji tunaokaa mtaa huo tukawa tunakutana pale , maana mimi home kwetu ilikuwa kama vile ndio sehemu ya "( makutano)"
Kwahiyo kuhusu nyimbo , uandishi , mazoezi kila kitu tulikuwa tunafanyia hapo , japokuwa wote walikuwa sio Wana muziki , wengine Enzi hizo walikuwa ni wadogo wadogo sana , na kipindi hicho Brother soggy doggy alikuwa Tayari amekwisha kuwa mwanamuziki mkubwa .
alikuwa Tayari amekwisha fanikiwa kutoa Kazi zake kadhaa , kwahiyo ndio mpaka kukutana na sisi , kwa maana sisi tayari tulikuwa na idea zetu tayari ..
tuna rap lakini Bado tulikuwa hatujui ni wapi? Tunaweza kupata chance ya kuwazirisha vipaji vyetu ..
Kwahiyo Brother " soggy doggy" Alipo fahamu kwamba sisi tuna vipaji , ukaribu ukazidi kuendelea zaidi na zaidi, na baada ya hapo tukaanza kufanya project za kundi ( crew ya hot pot family)..
Lakini hata hivyo wimbo wangu wa " vidonge vyao" kundi langu la " hot pot family" lilishiriki kwa kiasi kikubwa kuandika lycris akiwepo brother "soggy doggy" na kwa Bahati zuri mimi nikawa nimechanguliwa na producer master jay..
Producer master jay Enzi hizo Aliweza kutoa ofa , kwa sababu kipindi kile mimi nakumbuka ma producer walikuwa na Desturi ya kutembelea katika sehemu mbalimbali ambazo zilikuwa zina Desturi ya kuandaa kitu kinaitwa " talent show" kwenye maeneo kama vile hamana , kinondoni kule , kwenye ma concept za shule bilicanass nyakati za weekend,
Kwahiyo producers wengi Enzi hizo akiwemo master jay walikuwa wanakuja mule , wanashuhudia sisi tukiparform kwenye beat za watu za wasanii wa Ulaya..
Kwahiyo walikuwa wanakuja kutazama vijana wenye vipaji , na kwa sababu mimi nilikuwa karibu sana na brother " soggy doggy" kwenye matamasha mengi ya " talent show" nilikuwa naonekana sana na kuonyesha kile nilichonacho kwa watu.. nikawa nimepata Bahati na producer master jay akawa amenikubali sana kutokana na style yangu ya uimbaji, akamueleza Brother soggy doggy kwamba anataka kufanya Kazi na mimi.
Brother soggy doggy akadai hakuna noma ni fresh , kijana huyu hapa.
Baada ya hapo mimi ndio nikawa nimeenda kwa producer "master jay " nikaanza kurekodi huo wimbo wa " vidonge vyao" wimbo ambao ulikuwa umeandaliwa kwa usaindizi wa familia ya " hot pot family" akiwepo brother " soggy doggy"
Ilikuwa ni katikati ya mwaka 2001/ 2 kwa sababu pia huu wimbo ulikaa studio pale mj records Takribani kama miaka miwili ..
Watu wengi ambao tulikuwa tunashiriki katika hizi talent show , Tulikuwa tayari na idea ama vipaji ,
Nikizungumzia kitu kama " talent show" ndio ilikuwa sehemu maalumu tunakutana na wasanii na makundi kama vile...
"University corner", Ommy G, Daz baba ..
Generation yetu kwa kiasi kikubwa wengi walikuwa wanashiriki katika hizo " Talent show" kuonyesha vipaji vyao, kabla hawajarekodi , baada ya hapo kila mmoja aliweza kuonekana na kufikia muda na kuuanza kurekodi kwahiyo chimbuko lilikuwa kwenye hizo " talent show" Enzi hizo..
Na ni wengi tu katika Generation yetu waliweza kushiriki katikati hizo " Talent show" na zamani hiyo ndio ilikuwa sehemu pekee ya kukutana na washigaji, kwakuwa Enzi hizo hakukuwa na simu , simu zilikuwa ni za mezani Tu na sio kwamba watu wote Enzi hizo walikuwa na Uwezo huo wa kumiliki simu hizo.
Sehemu kubwa ambayo tulikuwa tunakutana sisi kama wasanii ilikuwa ni hizo sehemu za " Talent show"
Matamasha yale ya shule, matamasha ya mchana..
ni matamasha ambayo yalikuwa yanafanyika almost kila week ...
nilipata nafasi ya kwenda kwa master jay , lakini nakumbuka kipindi hicho producer master jay alifanikiwa ama alichangua watu Takribani kama saba hivi
Nikiwepo mimi Suma G, Ommy G, wakiwepo crew ya university corner ..
KWA wale wasio mfahamu msanii Ommy G hizi ni Baadhi ya nyimbo zake alizofanya hapa katikati Ommy G.
1. Rundi mwana
2. salama
3. choo cha kike
Enzi hizo kiukweli
kulikuwa na washigaji wengine walikuwa wanakaa mitaa ya tabata kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa " maliki" na alikuwa na jamaa yake mmoja anaitwa " dallaz" na crew nyingine ilikuwa inaitwa " necks breakers ...
Dallaz aliimba nyimbo moja inaitwa " mtaani kwetu ft banana zoro " kwahiyo dallaz na maliki ndio walikuwa wanaunda hilo kundi na walijiita " necks breakers"
Kuna watu kama saba hivi waliweza kupata hiyo nafasi ya kufanya Kazi moja moja kwa producer master jay pale mj records Enzi hizo..
Na kumbukumbu na hiyo Kazi yangu ya " vidonge vyao" nilimshirikisha jamaa yangu anaitwa " Ommy G"
Aliingiza vionjo kwa mbali kwenye chorus " waaah waaah..!!..?
Sinaujua msanii " Ommy G" alikuwa ana element flani kama vile marehemu " DMX"
Ndio huyo alishiriki na wimbo wangu ukawa umekamilika , lakini wimbo huo ulikaa sana studio , sikufahamu ni kwa sababu Gani , kwa sababu hapo tayari wimbo huo upo mikononi mwa producer master jay .( Project ya mj records).
Na mimi shahuku yangu kubwa ilikuwa ni kuwakilisha kile nilichonacho, Tamaa yangu kubwa kisikike kwa watu , maana Muziki Enzi hizo ulikuwa Bado kuwa sehemu ya biashara , tulikuwa na hamu tu ya kujulikana kisha hapo baadae tuje kutazama what next..
Mwaka 2003 nadhani hawa maproducer wakawa na Desturi ya kutembeleana katika studio zao na kusikiliza Kazi za wasanii mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti pale wanapopata chance ya kutembeleana..
Na kipindi hicho alikuwa amekuja producer mpya kutoka nje ya nchi..
yule producer alikuwa ana Asili ya mtu wa Asia anaitwa Amit Mental nadhani huyo producer alikuwa ana urafiki na producer master jay wakasikilizishana baadhi ya project lakini kipindi hicho tayari producer Amit Mental alikuwa amekwisha Fanya project kadhaa za wasanii hapa Bongo kama vile na msanii t.i.d na wimbo wake unaitwa " siamini"
Ambayo original version yake ilifanyika katika studio za MAWINGU chini ya producer & dj bonnie luv project za mwanzo kabisa miaka ya 1990..
Wimbo ambao T.I.D alichukua sampo ama idea na kutengeneza wimbo huu wa " siamini"
Kwahiyo aliposikilizishwa nyimbo yangu ya " vidonge vyao" na master jay akawa nae amevutiwa na mimi kupitia maybe floo & style kwahiyo na yenye akazungumza na master jay na kutaka kufanya maamuzi ya kufanya project na mimi
Nyimbo ya "vidonge vyao" kwa upande wangu ilikuwa ni idea tu lakini kiukweli hapa nyuma ilikuwepo Taarabu moja maarufu Enzi hizo inaitwa " vidonge vyao" alikuwa ameimba mama yetu mmoja anaitwa " Nasma hamisi kidogo" kwa Sasa amekwisha Tangulia mbele za haki kwa upande wangu mimi ilikuwa ni idea tofauti na msanii " inspector haruna" kutoka crew ya " gangwe mobb " ambao wao walimchukua kabisa yule mama na kueleza jamii kuwa idea ama sampo ya wimbo huo ni kutoka kwa marehemu " Nasma hamisi" mwimbaji wa Taarabu Enzi hizo..Sisi wakati tunaaza Game tulikuwa tunapenda sana kusikiliza Kazi za ma brother zetu ambao wamekwisha tutangulia kwenye Game ya Bongo fleva wasanii kama vile .
Mh Sugu , makundi mengine yalikuwepo Enzi hizo kama vile " wapambe nuksi" watu wa ilala kina " mack d" kina soggy doggy wasanii ambao walikuwa wametutangulia katika muziki wa Bongo fleva..
Muziki ulipopata nafasi ya kucheza nyimbo za Bongo fleva hao ndio wasanii wa mwanzo kabisa kazi zao kuchezwa katika vituo vya radio Enzi hizo hasa " "MAWINGU fm" Clouds fm .
Makundi kama kwanza unit , na kipandi hicho muziki wa Ulaya ulitawala sana.
Na mara nyingine tulikuwa tunainga Ama kutumia style za wasanii kutoka Taifa kama la Marekani wasanii kama kina 2 pac, nyimbo kama Dear mama nk..
Nyimbo kama ya mh Sugu inaitwa " nipo kwenye mic phone " nyimbo aliyomshirikisha fanani.., tulikuwa tunaingilizia nyimbo za ma brother zetu , tuna rap na mwisho wa siku na sisi tukapata nafasi na tukaonyesha Uwezo na kipaji kwa jamii, kama unaweza kuelezea kitu cha mtu kupitia lycris katika nyimbo huo ni Uwezo mkubwa sana kama msanii..
Cha kwanza mimi Tangu shuleni Mungu amenijalia kipaji cha kuimba na kuandika lycris, na style zuri ya kughani Tungo na mashairi yangu kwa ujumla..
Mpaka ikafika time watu wakawa wananipoint ama wananiita " Genius" maana vitu ambavyo nilikuwa nafanya sio kwamba nilikuwa nimesomea " Hapana!!!.. ni vitu tu ambavyo vilikuwa vinakuja outomatic , ni vitu ambavyo ulikuwa ukiviweka upande wa Elimu , vinaweza vikawa vinatoa Elimu kubwa sana kwenye jamii , maana nyimbo zangu nyingi zilijikita zaidi kwenye kuelimisha jamii ukisikiliza nyimbo kama vile " vituko uswahilini" , pombe ikikolea , sheria zimewekwa ili zivunjwe . Ni nyimbo nyingi tu ambazo nilikuwa nimetoa hapo awali nilikuwa nimesielekeza sana kwenye kuelimisha jamii , kukosoa kwahiyo sikusomea Muziki ni kitu ambacho Nimezaliwa nacho outomatic toka kwa Mungu kwenye upande wa Elimu nimeishia kidato cha nne tu " form four"
Enzi hizo niliweza kufanya vitu vyote kwa wakati sahihi kwenye upande wa Elimu na sanaa yangu ya uimbaji kwa ujumla Enzi hizo nikiwa Bado shuleni...
Namshukuru hata hivyo sikuweza kusoma sana zaidi ya Elimu ya kidato cha nne " form four"..
Elimu ya form four imenifanya kuimalika kiuchumi na kunifanya niweze kufanya shughuli zangu kiuzuri zaidi , kiukweli muziki haukuweza kunihadhili hadi kuweza Ama kupelekea kutoka kwenye Main line ama kwenye ramani ya maisha.
Kwanza kipindi hicho tulikuwa tuna nyimbo nyingi sana tunaandika katika madftari Yetu , kwahiyo na katika Generation yetu wasanii wengi tulikuwa tunaandika nyimbo katika madftari Yetu , unaweza ukajikuta una album nzima katika daftari lako wewe kama msanii lakini Bado ujapata chance Ama nafasi ya kurekodi studio.
Kulikuwa na changamoto nyingi na zingine kama hizo , na ndio maana tulikuwa tukipata chance ama nafasi ya kwenda studio kurekodi mara zote tulikuwa tumekwisha jiandaa muda mrefu sana kwahiyo tulikuwa na kiu ya kurekodi na ndio maana sisi wakati wetu kama wasanii wa zamani ukipata nafasi ya kwenda kurekodi ilikuwa ni "one take" inawekwa beat unapasuka mpaka Ngoma inakwisha ..hiyo ilitujenga kwa sababu tulikuwa tunajiandaa mapema Tofauti na wasanii wa sasa.
tunaandika vitu mapema kwahyo mimi nilikuwa na nyimbo nyingi tu ambazo kipindi hicho siwezi kusikumbuka zote kiukweli, na ndio nilikuwa natumia Enzi hizo. Kwenye majukwaa mbalimbali ya "Talent show" nikipata nafasi ya kuparform Kwa mfano pale hamana vijana center pale kulikuwa na Topic zinaandikwa , ambazo hizo topic zinawazirishwa kila j.pili ..
kwahiyo kwa mfano j.pili Hii kuna topic inasema " kijana anapaswa kuowa akiwa na umri Gani " inakuwa ni kama Agenda Ama Topic inayozungumziwa hiyo wiki siku ya j.pili .
Kwahiyo kila mtu anatoka pale na hiyo Agenda Ama Topic kwenda kuandika wimbo .
sasa akija msanii j.pili inayokuja anaiparform ile nyimbo ikiwa na ujumbe wa ile Agenda Ama Topic ya wiki iliyopita na pale tena kwenye notes board anaondoka na Agenda Ama Topic nyingine kwaajili ya kuandika wimbo mwingine kutokana na ile Agenda iliyowekwa katika ile notes board pale shuleni kwaajili ya wiki ijayo.
Kwahiy nalo hili lilitujenga na kuwa waandishi wa wazuri .
Maeneo ambayo tulikuwa tunapenda kwenda kuonyesha vipaji vyetu ama sehemu zilizokuwa zinaanda hizo show ama event za "Talent show" ni kama vile..
Hamana vijana center, kulikuwa na pale kinondoni pale asenti class , kuna ukumbi mwingine pia posta , ukiacha bilicanass kuna coloniani culture, mambo Club..
Na ndio sehemu kama hizi zilikuwa zinaanda matamasha ..
Wasanii tulikuwa wengi sana Enzi hizo kwahiyo tuliokuwa tunapata nafasi ni wachache mno.
Tulichoangalia sisi ni Aina ya watu tunaokutana nao pale na unawapima kwamba hapa niimbe nyimbo ipi? Ili niweze kuendana na mazingira na aina ya watu ama mashabiki waliohudhuria hilo Eneo .
Brother soggy doggy ndio mara nyingi nilikuwa nae na kuna kipindi brother soggy doggy alienda kufanya Kazi Mwanza kama radio prisenter katika kituo cha radio pale Mwanza kinaitwa " radio free Africa" ..
mimi nikawa nimeenda kule Kwa sababu ya ukaribu wangu na soggy lakini pia mimi na soggy doggy wazazi wetu wote walikuwa wanaishi sehemu moja inaitwa uwanja wa ndege , kwakuwa yenye Soggy doggy alinatangulia na mimi nilikuwa kama mdogo wake alikuwa ananiona nina Uwezo mkubwa kwahiyo akawa ana hakikisha kuwa na mimi kwenye kila point ama Eneo analosogea ,
Alianza kufanya Kazi Mwanza kisha soggy doggy akawa ameniita mimi nikaenda kukaa nae huko Mwanza almost kama miezi miwili hivi , nimekaa Mwanza nilikuwa nafanya interview nina floo Ngoma zangu ambazo sikuwahi kurekodi , kipindi hicho kina kind bway Enzi hizo wakiwa Wana host show ama kipindi pale " Radio free Africa.
Walikuwa wananifanyia interview mara kwa mara hadi pale nilipotoka kule na kurudi Dar es salaam ..
nilianza kufloo na kupata Experience hiyo kwenye radio nawekewa Beat , kwakuwa nilikuwa ni kitu ambacho nakifanya mara kwa mara ..
Kwa upande wangu lilikuwa jambo rahisi sana.
Mpaka baadhi ya watu kwenye mitaa na maeneo kadhaa jijini Mwanza wakawa wananihalika kwa kufahamu mimi ni msanii mkubwa..
Jina langu la kwanza la kinasanii walikuwa wananiita " G boy" nyani Gesta boy" jina lingine ni 2 pac wa hanasa kwa sababu nilikuwa napenda sana kuweka kilemba kichwani mtaani na kuvaa katakei kama marehemu 2 pac , kwenye mtaa wa tandika kule Kwa bibi yangu kuna mtaa unaitwa " mtaa wa hanasa" na mara nyingi nilikuwa naenda kule naishi kwa Bibi , kila mtu akawa ameniita " 2 pac wa hanasa" hanasa ndio jina la mtaa ninao kaa na 2 pac ndio jina nililokuwa najiita.
Kwahiyo nimetoka kwenye kutumia jina la G boy, 2 pac wa hanasa. Nyani Genius ndio lilikuwa jina la kwanza sema watu wengine kila mmoja aliweza kulitafsiri kwa uelewa wake ile herufi ( G) ..
Na sasa natumia jina la Suma Genius a.k.a silaha maneno,
Wimbo wangu wa vituko uswahilini ni maisha halisi niliyokutana nayo uswahilini..
Na ukizungumzia mtu kama mimi Suma G nimeishi uswahilini kwa kipindi kirefu , kwahiyo yale yalikuwa ni maisha tunayoishi nayo mtaani.
Maeneo nilioishi ni kama vile tandika, mangomeni kuna sehemu tadale , kuna mtokole wakati tukiwa wadogo Enzi hizo tunapitia maeneo hayo tukiwa tunaenda kucheza mpira tunapitia pita hizo sehemu mburahati , vingunguti ,kipawa.
Kwahyo mimi nilikuwa tayari nipo kwenye Muziki nikaamua kushare yale maisha ya uswahilini kama kituko kwa watu wengine kupitia sanaa ya Muziki..
Kiukweli ni maisha halisi na mpaka leo kuna baadhi ya vitu vinaendelea kutokea katika hayo maeneo. .
Nilikuwa naishi maeneo ya karakata maeneo ya kipawa kwa upande wa pili ila kuna mazingira ambayo mimi nilikuwa napita mara kwa mara na kuona vituko vingi vya Aina hiyo.
Lakini wimbo huo baada ya kurekodiwa na kutoka watu wa maeneo yale wakaaza kunimaidi sana na kudai kwamba mimi nimeimba maisha yao.
Kwahiyo kumbe kila unapopita kwenye haya mazingira yetu unaenda unatochora tu hadi umepelekea kutudiss kwenye mazingira yetu kupitia hiyo Ngoma ya " vituko uswahilini"
Nikawa nawauliza kwani mimi mwenyewe naishi wapi? Jamii mbona hata mimi daily Tupo na nyie Humu Humu uswahilini.
Ikapelekea hii Ngoma mpaka kuniletea beef kitaani na baadhi ya masela na wahuni kitaani hadi kutamani kumfanyia kitu kibaya kutokana na fikra zao kwamba nimewadhalilisha sana kuimba uhalisia wa mazingira wanayoishi.
Ulifikia watu wakanielewa lakini baadhi walipindi kukubali hivyo hivyo kishingo upande . Na baada ya hapo inapindi tumuache mwanaharamu apite na maisha mengine yaendeleee...
Maana kama ni ujumbe umekwisha fika kwenye jamii .
Ngoma ya Easy to the I inayoitwa " Dem wako ananitaka" ni True stori ambayo ilimpata jamaa yangu wa karibu ndugu Easy to the I
Alikuja Gheto nakunieleza kila kitu kwamba kuna dem wa jamaa yake anamtaka, lakini kama nilivyokueleza hapo mwanzo kwamba family ya hot pot family ilikuwa kubwa na sio wote walipendelea kuimba lakini kwa Easy to the I alijikuta akishawishika ama kama mkumbo fulani hivi wa kutaka kufanya muziki nae akaaza kupata hamasa na mwisho wa siku nae akatoa Ngoma.
Akanieleza halisi ya mapito anayopitia kutoka kwa hiyo Dem wa msela wake.
Hadi msela anadai anatamani kufikisha message ama ujumbe kwa jamaa ake kwamba Dem wake anamtaka.
Nami kama suma G nikamueleza mbona hii ni Bonge la mkasa ama idea kwanini tusiandike wimbo.
Kwakuwa Easy to the I alikuwa ajui kuandika mashairi , mimi nikamwambia andika matukio ama vitu vyote ama viashilia anavyokuonyesha yule Dem wa mshgaji kisha leta kwangu mimi niandike Ngoma .
Nami katika hiyo Ngoma nilitaka kuweka Chorus tu ila mwanangu Easy to the I akawa amekomaa sana na mimi niwekea verse yangu mule ili unibebe na mimi Enzi hizo tayari nimekwisha kuwa mtu maarufu kwenye hii industry ya muziki wa Bongo fleva.
Nikaa nimeandika lycris zote kisha tukaamua kwenda kwenye studio za sounds crafters kwa producer Enrico tukarekodi na ukatoka na kila mdau na shabiki wa muziki wa Bongo fleva kiukweli aliupenda wimbo huo.
Ngoma nyingine aliyoitoa ndugu yangu Easy to the I ni wimbo unaitwa " suti" ila haukufanya vizuri sokoni maana ukupewa Airtime sana na vituo vya radio Enzi hizo .
End...🔥🔥🔥🔥
HUYO NDIO SUMA G , SUMA GENIUS A.K.A SILAHA MANENO KIPAJI HALISI KUTOKA USWAHILINI
Follow na like Page yetu Facebook ya UKWAJU WA KITAMBO
Mawasiliano +255767542202