snipa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 4,437
- 2,043
Miongoni mwa underground wa hip hop aliyekuwa anachipukia (Suma mnazareti) kupitia label ya Lunduno siyo siri ali hit sana ! Na binafsi nilielewa sana kazi zake !
Nanukuu kutoka ngoma aliyoifanya mnazareti na Stamina ! ====> Agano Jipya
Nanukuu ''MISTARI IMEJAWA UBABU HAD MABABU WANAAMKIA/ HUYU BIBI KAITAKA RAP ATAKIMBIZWA HADI ATALIA''
wote tunakubaliana aliposema bibi ===> alimaanisha BiBi Cheka ! Kwamba kaitaka Rap hatoiweza na atakimbizwa mpaka atalia !
Lakini yeye sasa kaachana na Hip Hop aliyotumia Kumponda BiBi Cheka wa watu na kaifuata Bongo Fleva ! Huko nako kakimbizwa mpaka sasa anaelekea kulia ! Mana yupo kimya sana na hata akitoa ngoma itakuwa ya kawaida sana!
Baada ya kuukana muziki wa Hip Hop ambao Ndugu yetu huyu alikuwa anautendea haki !
Nakwenda kuvamia Bongo Fleva mwanzoni ali hit sana ! Ndiyo ni sahihi !
Lakini kitu kama hukiwezi hukiwezi tu !
Mana huko Bongo Fleva inabidi akawasifie tu Madem n.k ila siyo kama hip hop aliyotumia kumponda BiBi Cheka !
Najua kuna baadhi watapinga lakini huyu mnazareth kwenye Gemu kapotea ! Kabisa !
Na tusitarajie kabisa kama ataweza kurejea kupitia staili aliyokuja nayo !
Lakini sasa nadhani anaona Vizuri label ya Tamaduni Muzik (VITENDO ZIDI YA MANENO) ikizidi kupeta !
Pole Mnazareth