Suma Mnazareth Mpaka sasa Hajielewi elewi! Baada ya kuvamia Bongo Fleva !

Suma Mnazareth Mpaka sasa Hajielewi elewi! Baada ya kuvamia Bongo Fleva !

snipa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
4,437
Reaction score
2,043
suma-mnazaleti.jpg

Miongoni mwa underground wa hip hop aliyekuwa anachipukia (Suma mnazareti) kupitia label ya Lunduno siyo siri ali hit sana ! Na binafsi nilielewa sana kazi zake !

Nanukuu kutoka ngoma aliyoifanya mnazareti na Stamina ! ====> Agano Jipya

Nanukuu ''MISTARI IMEJAWA UBABU HAD MABABU WANAAMKIA/ HUYU BIBI KAITAKA RAP ATAKIMBIZWA HADI ATALIA''

wote tunakubaliana aliposema bibi ===> alimaanisha BiBi Cheka ! Kwamba kaitaka Rap hatoiweza na atakimbizwa mpaka atalia !

Lakini yeye sasa kaachana na Hip Hop aliyotumia Kumponda BiBi Cheka wa watu na kaifuata Bongo Fleva ! Huko nako kakimbizwa mpaka sasa anaelekea kulia ! Mana yupo kimya sana na hata akitoa ngoma itakuwa ya kawaida sana!

Baada ya kuukana muziki wa Hip Hop ambao Ndugu yetu huyu alikuwa anautendea haki !

Nakwenda kuvamia Bongo Fleva mwanzoni ali hit sana ! Ndiyo ni sahihi !
Lakini kitu kama hukiwezi hukiwezi tu !

Mana huko Bongo Fleva inabidi akawasifie tu Madem n.k ila siyo kama hip hop aliyotumia kumponda BiBi Cheka !

Najua kuna baadhi watapinga lakini huyu mnazareth kwenye Gemu kapotea ! Kabisa !

Na tusitarajie kabisa kama ataweza kurejea kupitia staili aliyokuja nayo !


SUMA.jpg

Lakini sasa nadhani anaona Vizuri label ya Tamaduni Muzik (VITENDO ZIDI YA MANENO) ikizidi kupeta !

Pole Mnazareth
 
huyu jamaa vipi tena? yaani bongo kuna wasanii wana zaidi ya miaka mitano kwenye game lakini bado ni UNDERGROUND.
 
Sura yake inapendeza kuimba kwaya, ndo maana bongo fleva haimtoi....
 
Kweli haka katoto kalukuja kwa kasi enzi zile lunduno ila baada ya kutimuliwa kimyaa hakuna cha ustadh juma walann kahit na kasingo kamoja tu kule watanashati
 
Sijawahi kumkubali,kimtindo kama alikuwa anaforce game,ila angetulia kwenye hip hop,but ndo hivo mziki wa bongo hamna ubunifu,mc anaweza kuotea wimbo mmoja au single moja akaotea na biti,basi atahit subiri sasa kinachofuata
 
huyu jamaa vipi tena? yaani bongo kuna wasanii wana zaidi ya miaka mitano kwenye game lakini bado ni UNDERGROUND.

Mfano halisi Tamaduni Music wanajua sana ila hawatatoka kamwe watakuwa underground mpaka wanazeeka
 
Back
Top Bottom