SUMAJKT yakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi millioni 50 Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo

SUMAJKT yakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi millioni 50 Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
SUMAJKT imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 50 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, Kitengo cha Mama na Mtoto, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto.

Akikabidhi Vifaa tiba hivyo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Shija Lupi, kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema vifaa hivyo vimepatikana kutokana na michango ya SUMAJKT MARATHON iliyofanyika mkoani Dodoma kwa lengo la kusaidia Huduma ya Afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Makole iliyopo Dodoma, na Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kitengo cha mama na mtoto Mwenge.

Brigedia Jenerali Lupi amebainisha kuwa kwa Hospitali ya Makole SUMAJKT ilifanikiwa kukabidhi Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya millioni 100.

Aidha, Brigedia Jenerali Lupi ametoa shukrani kwa wadhamini wote, Kampuni Tanzu za SUMAJKT pamoja na watu wote walioshiriki katika kufanikisha SUMAJKT Marathon.

 
Back
Top Bottom