SUMATRA! Msaada tuelimisheni daladala Dar

LIFE HELP

Senior Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
149
Reaction score
71
Bila shaka tunategemea na kumekuwepo na mabadiliko kadhaa ya sector hii ya usafiri Dar, sisi kama wadau wa hii huduma tungependa kuelewa nini taratitu/mwelekeo/Policy/Vision ya SUMATRA katika sector hii ya usafiri DAR kwa siku za usoni yaani miaka 2 hadi 10 ili kukamilisha na kuepuka yafuatayo: (Aidha anaye anza au alie ndani)

1.Kuepuka hasara tokana na uekezaji usio sahihi, usio fuata sheria na taratibu za mamlaka husika.

2. Kuepuka hasara / uharibifu wa rasilimali ambazo zingetumika sehemu nyingine mfano watu wana kopa Bank kununua Mini Bus kesho yake unamwambia haruhusiwi kupewa leseni n.k

3.Kuelewa ni muundo gani wa Biashara/Kampuni (Organization Type) unao stahili au kukidhi taratibu na sheria zote za mamlaka, Mfano; kampuni –LLC, Shirika- S Corporation, C Corporation, Sole Proprietor, Partnership, Co-operatives, Join Venture..n.k.

4.Kuelewa ni kiasi gani cha uwekezaji (investment) kinachostahili ili Shirika au kampuni isajiliwe kufanya biashara hiyo, kwani kumekuwepo na usemi mitaani aidha matangaazo yenu kuwa Mamlaka HAITA SAJILI mtu mmoja mmoja, Pia ITASAJILI TU KUANZIA MAGARI KUMI NA kuendelea

5.Ni gari/bus aina gani zitakazo ruhusiwa kusajiliwa labda pia tokana na maeneo mbalimbali yaani zenye uwezo wa abiria wangapi minimum(seats) ? labda type za body aidha milango n.k.

Tumeamua kutumia jukwaa hili baada ya juhudi zetu za kutafuta taarifa hizi muhimu kwetu kugonga ukuta baada ya kila tunapofika ofisi za SUMATRA hatupati majibu aidha mhusika yuko vikao leo na kesho n.k. mimi sio msemaji subiri Fulani, nenda makao makuu n.k.

Nadhani pia ni jambo la busara kuwandaa wazalendo/wazawa ili kumiliki uchumi wao kuliko ghafla wawekezaji toka nje wanaingia kwenye shughuli/biashara ambazo hata sisi wenyewe tunaziweza.

Inaendelea kujengwa.....
 
Tatizo Tanzania hatuna long term plan au frame work structure inayotuongoza kufanya,
Uchumi unaongozwa na wenye nazo na ndio hao wanaoleta hizi surprise plans/projects ambazo zinatuumiza sisi wenyewe.
Mfano huu mradi wa mabas yaendayo kasi kwa hapo dar, ukichunguza kwa makini ni mradi tu wa wenye nazo kwani tunashindwa nini kuwa na project ya kujenga barabara zinazokidhi mahitaji? Kwa nn hakukuwa na mpango wa miaka mia au 200 baadae? Ina maana hatuwezi kuplan au?
Makosa hayasahihishwi tunaendelea nayo, nenda bunju au maeneo yoyote ambayo yanajengeka kwa sasa angalia utaratibu ulivyo ni yale yaleee ya enzi ambapo mwisho wa siku hata barabara haiwezi kukidhi haja.
Kaka pole sana na najua wengi wataumia kwa hili.
Tatizo ni mfumo mzima na sio Sumatra peke yake wao ni watekelezaji wa sera usiwalaumu saana.
We have long way to go....!
Inauma sana
 
Watu walitaka kuuza nyumba zao kigamboni wengine walitaka kujenga hayo yote kwa sasa yamesimama eti mji mpya mwaka wa ngapi sasa hatuoni matokeo yoyote...lack of vision ya uongozi wetu...mambo ya sumatra ni matunda ya uongozi mbovu uliojuu....mambo yaliaribika juu sasa system yote is collapsed...najua usumbufu waliopata watu wa daladala...changamoto ni kubwa ushauri ni kutafuta route mpya...
 
Bila shaka tunategemea na kumekuwepo na mabadiliko kadhaa ya sector hii ya usafiri Dar, sisi kama wadau wa hii huduma tungependa kuelewa nini taratitu/mwelekeo/Policy/Vision ya SUMATRA katika sector hii ya usafiri DAR kwa siku za usoni yaani miaka 2 hadi 10 ili kukamilisha na kuepuka yafuatayo: (Aidha anaye anza au alie ndani)

1.Kuepuka hasara tokana na uekezaji usio sahihi, usio fuata sheria na taratibu za mamlaka husika.

2. Kuepuka hasara / uharibifu wa rasilimali ambazo zingetumika sehemu nyingine mfano watu wana kopa Bank kununua Mini Bus kesho yake unamwambia haruhusiwi kupewa leseni n.k

3.Kuelewa ni muundo gani wa Biashara/Kampuni (Organization Type) unao stahili au kukidhi taratibu na sheria zote za mamlaka, Mfano; kampuni –LLC, Shirika- S Corporation, C Corporation, Sole Proprietor, Partnership, Co-operatives, Join Venture..n.k.

4.Kuelewa ni kiasi gani cha uwekezaji (investment) kinachostahili ili Shirika au kampuni isajiliwe kufanya biashara hiyo, kwani kumekuwepo na usemi mitaani aidha matangaazo yenu kuwa Mamlaka HAITA SAJILI mtu mmoja mmoja, Pia ITASAJILI TU KUANZIA MAGARI KUMI NA kuendelea

5.Ni gari/bus aina gani zitakazo ruhusiwa kusajiliwa labda pia tokana na maeneo mbalimbali yaani zenye uwezo wa abiria wangapi minimum(seats) ? labda type za body aidha milango n.k.

Tumeamua kutumia jukwaa hili baada ya juhudi zetu za kutafuta taarifa hizi muhimu kwetu kugonga ukuta baada ya kila tunapofika ofisi za SUMATRA hatupati majibu aidha mhusika yuko vikao leo na kesho n.k. mimi sio msemaji subiri Fulani, nenda makao makuu n.k.

Nadhani pia ni jambo la busara kuwandaa wazalendo/wazawa ili kumiliki uchumi wao kuliko ghafla wawekezaji toka nje wanaingia kwenye shughuli/biashara ambazo hata sisi wenyewe tunaziweza.

Inaendelea kujengwa.....

Shukrani mkuu utakuwa umetusaidia sote wadau wa sector nzima ya daladala kote nchini..
 
nafikiria bado,mie humo sijaingia kwenye Daladala,ila hii issue ya Darts na Uda ndio naona mwakani inaweza kuuwa soko
 
Back
Top Bottom