Sumatra ! Sumatra ! Msaada tuelimisheni daladala dar

Sumatra ! Sumatra ! Msaada tuelimisheni daladala dar

LIFE HELP

Senior Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
149
Reaction score
71
Bila shaka tunategemea na kumekuwepo na mabadiliko kadhaa ya sector hii ya usafiri Dar, sisi kama wadau wa hii huduma tungependa kuelewa nini taratitu/mwelekeo/Policy/Vision ya SUMATRA katika sector hii ya usafiri DAR kwa siku za usoni yaani miaka 2 hadi 10 ili kukamilisha na kuepuka yafuatayo: (Aidha anaye anza au alie ndani)

1.Kuepuka hasara tokana na uekezaji usio sahihi, usio fuata sheria na taratibu za mamlaka husika.

2. Kuepuka hasara / uharibifu wa rasilimali ambazo zingetumika sehemu nyingine mfano watu wana kopa Bank kununua Mini Bus kesho yake unamwambia haruhusiwi kupewa leseni n.k

3.Kuelewa ni muundo gani wa Biashara/Kampuni (Organization Type) unao stahili au kukidhi taratibu na sheria zote za mamlaka, Mfano; kampuni –LLC, Shirika- S Corporation, C Corporation, Sole Proprietor, Partnership, Co-operatives, Join Venture..n.k.

4.Kuelewa ni kiasi gani cha uwekezaji (investment) kinachostahili ili Shirika au kampuni isajiliwe kufanya biashara hiyo, kwani kumekuwepo na usemi mitaani aidha matangaazo yenu kuwa Mamlaka HAITA SAJILI mtu mmoja mmoja, Pia ITASAJILI TU KUANZIA MAGARI KUMI NA kuendelea

5.Ni gari/bus aina gani zitakazo ruhusiwa kusajiliwa labda pia tokana na maeneo mbalimbali yaani zenye uwezo wa abiria wangapi minimum(seats) ? labda type za body aidha milango n.k.

Tumeamua kutumia jukwaa hili baada ya juhudi zetu za kutafuta taarifa hizi muhimu kwetu kugonga ukuta baada ya kila tunapofika ofisi za SUMATRA hatupati majibu aidha mhusika yuko vikao leo na kesho n.k. mimi sio msemaji subiri Fulani, nenda makao makuu n.k.

Nadhani pia ni jambo la busara kuwandaa wazalendo/wazawa ili kumiliki uchumi wao kuliko ghafla wawekezaji toka nje wanaingia kwenye shughuli/biashara ambazo hata sisi wenyewe tunaziweza.
Inaendelea kujengwa.....
 
Back
Top Bottom