Sumaye apinga SERIKALI TATU

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,456
Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.

chanzo: BBC

Angalizo: Nadhani ana hoja
 
hivi huyu naye ni mhariri?fani imevamiwa...!
 
Mtu yeyote anayeitakia mema nchi hii hawezi kukubali serikali 3
 
kama tunataka muungano ni aidha serekali moja ama mbili, laa sivyo ya ussr yatajirudia kuna raisi atakosa nji ya kuongoza!
 
Muungano gani halafu serikali ziwe tatu, inatakiwa serikali 1 kama haifai basi na muungano haufai bora uvunjwe
 
Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.

chanzo: BBC

Angalizo: Nadhani ana hoja
Akili ya Sumaye ilishachoka siku nyingi, alishawahi kuhojiwa ni kwa nini Tanzania ni maskini akajibu hata yeye hajui ni kwa nini, imagine miaka 10 kama Waziri Mkuu hujui nchi ni kwa nini maskini ulikuwa unafanya nini kwenye hiyo nafasi?

Rasimu ya katiba mpya ni maoni yetu Wananchi yeye akafie Uyole kama anadhani hizi bado ni enzi za haambiliki.
 
mkuu nakumbuka mkwerre ndo kaulizwa hilo swali na sio Sumaye.
 
Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.

chanzo: BBC

Angalizo: Nadhani ana hoja

Kuna watu wameshaanza tayari ,nina uhakika watu hawa wanatumiwa.
Wanapinga Rasimu ya Serikali tatu kwa kigezo cha Gharama.
Eti Nchi itakuwa na Gharama Kubwa ku Run na Marais wa Tatu.
Watu kama hawa wanastahili Kukumbushwa kuwa kwa Sasa Nchi ina Ma Rais wa Tano na Wa Tatu wanatokea zanzibar.
Watu hawa wamekuwa wapofu kuona kuwa Tume ya Warioba imependekeza Baraza lenye Ma Waziri wasiozid 15.
Kwa Sasa Baraza lina Zaid ya Mawaziri 45, Mbona hawasemiGharama kubwa za ku Run the Current Baraza la Mawaziri?????
Hawaoni kuwa kwa Kupunguza Baraza la Mawaziri Mpaka 15 tUtakuwa tumeokoa Kiasi kikubwa sana Cha Fedha.
Watu wanaopinga Serikali 3 Hawastahili kuishi Tanzania,
TUSIMAME KUWAPINGA HAWA WACHUMIA TUMBO
 
Sumaye inaonekana anataka serikali 2 kwa kuwa anadai kama mungano wa sasa una matatizo yatatuliwe. Kwa mtazamo wangu hana hoja. Serikali mbili maana yake kwangu ni Tanganyika (TAN) na Zanzibar (ZNZ). Kwangu mimi mungano wa sSa umepitwa na wakati.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
mkuu nakumbuka mkwerre ndo kaulizwa hilo swali na sio Sumaye.
No data no research no right to speak, wa kwanza kuulizwa swali hili alikuwa ni Sumaye ila sikumbuki alikuwa nchi gani ya Ulaya, lakini alikuwa tayari ni Waziri Mkuu mstaafu. nina hakika na hili kwa asilimi 1000.
 
Mnaosema iwe serikali moja basi iwe ni serikali ya mapinduzi ya zanzibar sisi zanzibar tumepindua sio kama nyinyi kwa makaratasi na mnaosema serikali mbili basi iwe jamhuri ya watu wa zanzibar na jamhuri ya tanganyika kisha kama mnataka kushirikiana basi tucheki mambo fulani tushurikiane kwa mikataba maalum hafu mi nashangaa mbona watu wa tanganyika kila tukipapatua mupate serikali yenu hamtaki kwanini mnaogopa
 
Hivi mliwahi sikia kua pemba na unguja imeungana hivi visiwa ni vimoja tangea hiyo tanganyika haipo so huo wenu ni uchochezi
Visiwa hivi ukisikia ni vya aljazeera ambavyo nabii suleiman alikua akivitumua ni hivi hivi. Sisi tunataka tutengane na nyinyi tukae kivyetu
Variompa corione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…