Hafai na anamikono michafu, nilitegemea katika conference yake angeanza kwa kuwaomba radhi watanzania na kukubali kwamba ukiwa nje ya madaraka unaona zaidi kuliko ukiwa kiongozi manake yake yeye na Ben walikuwa vichwa ngumu kusikia watu wanasema nini.
Kukumbushia azimio la Arusha leo ni uvivu wa kufikiri kwani zipo namna nyingi ya kupelekea maendeleo na mawazo mapya ndio yanahitajika zaidi. Ukitafisha leo mali za watu binafsi na kuleta ujamaa si tu utaua nchi bali utaleta na vita, viongozi kuwa wafanyabiashara ni kuleta mgongano wa maslahi mfano ni yeye mwenyewe na soko la kibaigwa bila kuwa kiongozi angejuaje litajengwa soko na kuwahi kuwekeza kabla ya soko matokeo yake ni kutumia madaraka ili kulinda maslahi.
Wito kwa viongozi wastaafu kwa wawaombe radhi watanzania na kukubali kwamba wao ni sehemu ya chanzo ya msoto wote huu wanaopata wabongo. Pia wakubali wanatakiwa kusikia wakiwa madarakani sio kuziba masikio na kuona wao wanajua kila kitu wakitoka ndio wanataka kuanza kukosoa wenzao ambao ni matunda ili wasilaumiwe.
Kuwa waziri mkuu miaka 10 inatosha sana na wengine wapate fursa ya kuongoza yeye inatosha, mambo ya museveni bongo hatutaki.