Sumaye ndani ya Uingereza!

Status
Not open for further replies.
Kuna mtu kazungumzia kuhusu miaka 48 ya uhuru na bado tunapeleka viongozi kwenda kuangaliwa afya zao kwa watawala wetu. Mimi naona mtindo huu kuwa mwendelezo wa ujinga wa Mwafrika na ni ushahidi tosha kuwa Miafrika haiwezi kujitegemea yenyewe.

Kila siku tunapokea misaada kutoka kwa wazungu. Hiyo misaada inasaidia nini hasa na inamsaidia nani maana maisha tunayoishi sisi Miafrika na kusikitisha. Najiuliza hapa tusipopata hiyo misaada maisha yetu yatakuwaje?

Tungekuwa na akili kama mnavyodai baadhi yenu basi mambo madogo madogo kama ya tiba na mengineyo tungekuwa tumeshayamudu zamani za kale. Mtu gani mwenye akili anaweza kuishi maisha kama waishio Waafrika? Tunajidanganya eti tuna rasilimali kibao tu za kutuletea maendeleo. Okay, sasa kwa nini tuko mafukara? Kwani tumewekwa hapa duniani jana? Tuko hapa duniani since the beginning of times (whenever that is) na tumeshindwa kuyamudu mazingira yetu na kuboresha maisha.

We are just a lost cause. Kuna nchi ngapi za Ulaya (supposedly) zisizo na rasilimali nyingi kama tulizonazo sisi lakini ukiangalia viwango vyao vya maendeleo vimetuacha kwa mbali tu.

Aaaaah sisi tuna matatizo kweli.
 

Mkuu Tanzania is a secular state, kwa maana serikali na dini(na taasisi zake zote) zime tenganishwa. Tanzania haiendeshwi kwa sheria za kiislamu wala kikristo. Kwa maana hiyo basi hauwezi kutegemea kila sheria ambazo zipo kwenye Uislamu ziwepo serikalini, mfano umesema pombe, kama mtu anatoka dini ambayo haikatazi pombe? Ukristo una kataza kuwa na wake wengi, je Waislamu wakatazwe kuoa wake zaidi ya mmoja kisa imani ya mwingine?

Kuhusu chama cha Kiisalmu, narudia kua Tanzania is a secular state. Kama Tanzania ni secular chama cha kidini kitoke wapi sasa? Wewe hauna tofauti basi na hao viongozi unaowasema kwa maana unataka nchi iongozwe kama unavyo taka wewe. Vikianzishwa vyama vya Kiisalmu na dini zingine zikaanzisha vyama vyai nchi ita kalika? Serikali inaongozeka?

Mimi naona wewe hauna tofauti sana na unaowasema. You are just an opportunist trying to take advantage of current topics to push your agenda. Uliwasema mafisadi vizuri kwenye post ya mwanzo ila post hii imeonyesha dhahiri wewe ndiyo wale wale. Kama Uislamu umekusaidia kuwa mtu bora ni vyema ila usi sukume sheria za kiisalmu kua za kiserikali au sijui kuanzishwa kwa vyama vya kisiasa vyenye udini.
 
...am not CCM.ninavyoona mtandao ulivyo...Sumaye hana ubavu kuchukua fomu sasa kupambana na JK...ask him to try!!!

....... ninvyokumbuka alisema yeye siasa basi anakwenda kulima kwani ndio proffessional yake....kama kabili ok...tumpe nafasi...!!!..kuna tetesi kuwa ardhi kuanzia Kisarawe inayounganisha Kibaha amechukua yeye...mwenye data zaid anaweza weka....kama Kweli basi Sumaye atujuze amelitumiaje hilo pori!!!!

Kama yeye ana mission ya U-Rais kwanini asianze kuwa mfano wa kuigwa wa kuchekiwa Home TZ?... unavyomlalamikia JK kusafiri...dont u see this is part of it?...kwa nauli yake tu vinaweza nunuliwa baadhi ya vifaa vya kuanzia... i do believe kama Kiongozi mpenda wananchi wake...anaweza fanyiwa check hapa hapa tz....na unaweza kuwa mwanzo wa viongozi wengine kuchekiwa hapa. Kwenda zake Nje hakuna tofauti na Misafara ya JK....kama kuna Viongozi wengne wanakwenda..nao pia waache tabia hio....

kwa utaratibu huu tusiwalaumu Madaktari wetu kutokomea NJE kutafuta maisha yao.

Kwa Jinsi nilivyosema post mbalimbali humu JF...people are not serious kuupiga vita Ufisadi...Kumbe tuna majina ya Viongozi ambao wapo Nje ya cicle ya utawala....ambao nao pia ni Mafisadi!!!
 

Nakubaliana na wewe kuwa viongozi wetu wana takiwa kuwa mfano. Nakubaliana na wewe kuwa hizo safari za nje ziona gharama. Lakini tatizo siyo Sumaye tatizo ni sheria zilizopo. Cha kuangalia ni je Sumaye alicho fanya kavunja sheria? Privileges zote za waziri mkuu mstaafu ziko listed. Kama kuna tatizo basi sheria ndiyo ibadilishwe. Kuna mtu anakataa privilege anayo/aliyo pewa? Hata ingekua wewe mfano, kazi yako inakupa mafao fulani utaya kataa? Hakuna maana kum lalamikia Sumaye kwa maana ana tumia kilicho ainishwa na katiba yetu wenyewe. As long as kafanya kitu ndani ya katiba hata tulalamike vipi haja fanya kosa. Cha kufanya ni watu tuseme viongozi wetu au viongozi wetu wastaafu privileges fulani zipunguzwe au ziondolewe. Sawa a leader ana takiwa awe na moral conduct ya kukataa labda baadhi ya vitu. Akikataa sawa ni vyema ila asipo kataa hizo privileges bado haja vunja sheria.
Narudia, tatizo si Sumaye tatizo ni sheria. Kama sheria zina upendeleo mno ni jukumu letu kulalamikia zibadilishwe ila tukianza kulalamikia mtu mmoja mmoja hatu fiki popote na wala haitokua solution permanent. Sheria na katiba ya nchi ni sheria na katiba ya nchi mpaka hapo itakapo badilishwa.
 
..ni kweli kabisa pensheni wanazopata viongozi wakuu wastaafu ni kubwa mno.

..sasa imefikia mpaka Maraisi wastaafu wanajengewa majumba ya kifahari. tena wanakabidhiwa majumba hayo kuwa mali yao na familia zao.

..kama tumechochwa na ufujaji wa pesa za umma, kwa jina la mafao ya viongozi wakuu wastaafu, basi tuelekeze nguvu zetu ktk kusisitiza kwamba mafao hayo yarekebishwe kwa WASTAAFU WOTE. katika kufanya hivyo tuepuke ku-target watu fulani fulani kwa kusukumwa na imani za DINI.
 
Last edited:

Ngabu:

Ukiona mwafrika anafanya vizuri hiyo ni exceptional. Lakini wengi wetu tunaboronga.

Tunawacheka mababu zetu kwa kuita kuku wa kizungu au ng'ombe wa kizungu. Lakini ukweli wa mambo unabakia palepale kuwa viongozi wetu wanafuata check-ups na medical attentions za kizungu na sio sayansi ya medicine yenyewe.

Na kuonyesha jinsi tulivyofubaa kimawazo, mtu anamtetea JK, Mkapa, Mwinyi au Sumaye kwa sababu za kidini. Hii affinity ya kidini ni ya kipumbavu sana. Entitlements zao zinawafanya watu wa dini zote kuishi maisha duni.
 

Huko kulalamika si lazima kuanzie mahala? Si lazima tuwe na mifano ya namna hizo sheria zinavyoweza kuwa abused? Sumaye hapa anatumika kama mfano wa hao wengine.

Hata hivyo hao viongozi hawawezi kukwepa lawama. Kama Zakumi alivyohoji, kwani lazima kwenda uingereza? Kwa nini wasiende Kenya, Afrika Kusini, Cuba au India? Na je, akisema kuwa yeye atafanyiwa check-up Muhimbili atachukuliwa hatua? Tunachodai ni empathy kwa upande wa viongozi wetu. Kitu ambacho kiko in short supply.

Amandla......
 

Nadhani atakayeelimika na mjadala huu ni Sumaye siku zijazo atafanya linalompelekea sio kuchezea kodi za wananchi.

Viongozi kama hawa wanaweza kutumia maji ya UHAI au Kilimanjaro ya kunywa na kumwagilia bustani zao kwa kisingizio cha kuwa wana haki kikatiba.he should use our limited resources wisely sio KU ABUSE.

awe yeye,awe mzee MWINYI nitasema kama watakwenda kinyume na kutumia kodi zetu vibaya.

Sumaye hajui kama kuna watu wameuawa na mabomu Mbagala? kulikuwa na ulazima gani wa yeye kusafiri wakati hana anachoumwa?ameshindwa hata kwenda kuwapa pole wahanga wa mabomu.IBADA gani itapokelewa ya mtu mchafu wa namna ya Sumaye?

arudishe mashamba ya watu kibaigwa ndio ibada yake itakuwa na maana.
 

Waende Kenya? Kuna nini Kenya wakati hata wao viongozi wao wanaenda kwa wazungu? Na huko Afrika Kusini bila wazungu wala kusingekuwa kulivyo. Cuba na kwenyewe kume lost tu. Wa Cuba kibao wanapanda mitumbwi kwenda Marekani. India..puhleaaase..kwa majanjanja huko
 

Wanashindwa kuelewa mwanzo wa hesabu ni moja.ufisadi kaanza Mramba,akaja Yona halafu Mgonja. who knows watakuja wengine wanaweza kuwa Mkapa au Sumaye, lakini kama watu wangelalamika kuwa kwanini Mramba wakati wako kina Sumaye tusingeanza safari ya kuwashughulikia mafisadi.

kuna kina Rukaza na Maranda nao kwenye Epa wameanza watakuja wengine, na mimi nimeanza na hili la Sumaye kama kuna wengine watakuja.

watu wengi hapa wameshindwa kuelewa kuwa ninacholalamika mimi kuwa kama Sumaye alikuwa mgonjwa wa kuepelekwa UK,asingeweza kuwa anazurura mji baada ya mji kuhubiri neno la Bwana.angetembelea makanisa ya LONDON kwa ajili ya Ibada,za yeye ni MLUTHERI kule alikokwenda hakuna kanisa lake jaribuni ku google.sasa kama alikuwa na nguvu za kuzurura mkoa hadi mkoa,asingelilia kwenda nje kutibiwa yaani ugonjwa wake haukuwa serious.utapeli wake wa kusema kuwa anaumwa na apelekwe nje hapo ndio ninapolia nae.

amewahi kwenda Marekani kwa shughuli za kanisa ile sawa,lakini safari hii kasema akatibiwe na ameomba wiki nne awe UK.kama hakuwa serious na ugonjwa angekaa nyumbani.walinzi na yeye wanalipwa pesa za nje ya kituo cha kazi.

kuna Mchungaji MBEYA ALIKATAKAA kupokea sadaka za viongozi mafisadi.tusitumie makanisa vibaya.
 
Thread hii haina akili, imekaa kimajungu na kidini.

EPA ilipopelekwa bungeni kwa mara ya kwanza walijibu kuwa ni majungu.

MKONO aliahidi kuwashitaki watu kwa kumchafulia jina lake pale MwembeYanga. jee alikwenda mahakamani?alisema ni majungu na chuki.

Richmond nayo ilisemwa ni majungu na harufu ya udini rejea ripoti ya kamati ya Mwakyembe ipo humu. udini hutumiwa kufunika uchafu kama members wengi wanavyofanya kwa sumaye hapa.

kama unaona haina akili yanini umesoma na kuijibu?basi nawe huna akili na mtu wa majungu.

THE BOTTOM LINE SUMAYE KATUMIA KODI KWENDA KUHUBIRI INJILI,unapofanya jambo la Mungu zile nyenzo ziwe za halali sio wizi au kodi ya wananchi wanaouchukizwa na matumizi ya kodi yao.
 
Nimetatizwa kidogo alikwenda kutibiwa au kuangaliwa afya?
 
Sheria za madini zilikuwa na mapungufu Mengi kiasi cha kuunda tume ya jaji Bomani kupitia mikataba yote ya madini.case study au chanzo chake ni mkataba mmoja tu wa machimbo ya BUZWAGI.kila kitu kina chanzo kwenye hili wa kwanza ni sumaye.

lakini lazima uelewe ilitakiwa Sumaye aitaarifu serikali toka nyumbani kuwa "nakwenda UK kutibiwa na pia kuhubiri injili"

hakusema kuwa atakwenda kuhubiri Injili kwa hiyo system haitambui ziara zake za mahubiri kwenye miji mbali mbali ya UK.kwa hili kama usalama wa Taifa watafanya kazi yao basi walinzi wake wanaweza kujikuta kwenye matatizo.kiongozi hajiendei mahala ndio maana ya kupata clearence mambo ya nje kabla ya kusafiri.

kwa usalama wake huko alikokwenda kwenye mahubiri unaweza kukuta jengo walilokwenda halijasajiriwa kama nyumba ya ibada na kikimtokea kitu ni serikali yetu ndio itakayowajibika.

amevunja hadi protocol yake,yeye ni dipomatic hatakiwi kufanya mambo kienyeji.
 

Hakuna imani za kidini tunasukumwa na uzalendo kwa nchi yetu,Zubeir Zitto Kabwe ni muislam akaulalamikia mkataba wa Buzwagi uliosainiwa na Nazir Karamagi ambaye ni muislam.

DR.Mwakyembe ambaye ni mkristu alipendekeza waziri mkuu Lowassa achukuliwe hatua huku akiwa mkristu mwenzake.

tunajadili kama watanzania wenye uchungu na kodi zetu,kama wewe ukitizama kuwa anajadili fulani yuko dini yako unamtetea utakuwa unakosea ufisadi hauna dini wala kabila.
 
sumaye sheria ya protocal hamruhusu kuzurura ovyo, kumfuatilia sio none of our business kwani anatumia kodi yetu lazima awe answerable kwetu. Huoni wabunge wa uingereza wanavyowajibika hata kwa kutumia toilet paper ovyo.

Uko ulaya unashindwa kujifunza wabunge kila siku wanajiuzulu kwa matumizi kama ya sumaye uwe unasoma daily teleghaph lipo online uone watu wanafukuzwa kazi na spika anaondoka june 21 kwa vitu vya ulaghai kama kina sumaye.
 
We we Boma nchi inaendeshwa na katiba na sheria kama viongozi wako entitled na hizo rights huwezi walalamikia wakizitumia, for your info;Salim , Msuya, Warioba, Malecela and the list goes on to Kawawa wanatunzwa na Serikali, tena huyu Kawawa (jirani yangu), nyumba yake ambayo hakai inalindwa masaa 24 na huduma nyingine kede kede. Mwacheni atumie mafao yake ya Uongozi awe fisadi au la hiyo ni haki yake inayoendana na wadhifa.
 
kanda2,

..kwani Sumaye alifanya mahubiri mangapi, na ktk miji mingapi huko UK?

..viongozi wengine wakuu wastaafu pia wanashiriki ktk shughuli za kidini. nakumbuka Mkapa alikuwa Iringa kwa Waluteri, wakati yeye ni Mkatoliki, na nina hakika alikuwa chini ya uangalizi na matunzo ya serikali. je, Mkapa naye anastahili kushutumiwa kama Sumaye?
 

Sasa hapa ndugu yangu si ume dhihirisha wazi kuwa tatizo lako siyo kuwa kaenda nje bali kua kaenda nje aka hubiri dini. Si ungesema tokea mwanzo kuwa tatizo siyo kuwa kasafiri nje bali kasafiri na aka hubiri dini?
Una uhakika gani kuwa hakutoa taarifa kuwa ataenda kuhubiri mkuu? Are you his security detail? Labda useme kama wewe ndiyo moja wapo ya watu wanao husika na ulinzi wa wakuu na hukusikia katoa detail hiyo. Kiufupi lete ushahidi hakutoa taarifa hiyo.
Kiongozi yoteaki pangiwa security detail they can not anticipate everything. Kiongozi anaweza kwenda mahala halafu ikatokea shughuli ya ghafla. Kuna mtu maisha yake yanaweza kuwa staged kwa asilimia 100% mkuu? You can not tell me security detail haiwezi kumaccomodate kiongozi iwapo ratiba ita change. Kwa unavyo ongea wewe ina maana basi ikitokea jambo lolote dogo hao security detail hawana uwezo wa kumlinda.
Why are you so concerned about usalama wake hata hivyo? Umeanza kuipondo safari yake ya nje kisha uka hamia na kusema kwa nini kaenda kuhubiri sasa unasema kwa usalama wake mwenyewe. Is it any of your business ana lindwaje? Wakati umetoka kusema ana fuja pesa za walipa kodi.

Acha kuji changanya mkuu. Umeanza kulalamika kwa nini afanyiwe check up nje kisha tatizo ikaja kuwa aka fanya na mahubiri then ukaja kusema hakutoa taarifa sahihi kwa security detail(bado hatujaona ushahidi) then ukaanza kujidai you ae worried about his security & well being. Usi tufanye watoto. Wewe bainisha wazi ni nini haswa kuhusu hii safari ina kusumbua badala ya kuwa kigeugeu.
 

ana haki zote za kulindwa na kutibiwa ila ASI ABUSE system.ukiweza soma makala ya Majjid Mjengwa kwenye gazeti la Kwanza Jamii la tarehe 19 may.ameeleza mfano wa viongozi waadilifu wako vipi.mzee KAWAWA ni kati ya watu wanaotumia rasilimali au kodi zetu kwa umakini mkubwa sana,historia itamkumbuka kwa uadilifu wake.wadhifa hauendani na ufisadi wala mahubiri ya neno la bwana yanakataza ufisadi, hakuna point ya yeye kwenda kanisani huku mafundisho ya kanisa yanakataza ufisadi na kupupia mali za wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…