chuma said:
...Ninavyojua ukiwa Ndani ya nchi ya Tanzania sio Ufisadi...JK tunamlalamikia kwa kuwa anakwenda zaid Nje ya Tanzania...lau kama angalikuwa anatembelea mikoa ya Tanzania kelele zinazopigwa sasa zisingalikuwepo...!!!
au labda mwenzetu unatafuta justifications kwa bro Sumaye!!!
Chuma,
..sidhani kama safari za ndani haziwezi kuingia ktk UFISADI. kama Kiongozi wa serikali atatumia safari na shughuli za kiserikali kukipigia debe chama chake wananchi wanaweza kuwa na haki ya kudai huo ni UFISADI.
..kwa upande mwingine wako viongozi wastaafu ambao wameshiriki/wanashiriki shughuli zilizoandaliwa na taasisi za kidini. sasa tunachouliza ni kwanini hao hawapigwi vita wakati tunaelewa kwamba wanaishi kwa kodi ya wananchi?
..tunachojaribu hapa ni kuwa even handed. hata Polisi anaposhughulikia wahalifu anatakiwa afuate maadili, haki, na sheria. imewahi kutokea Polisi wakaadhibiwa kwa kutumia mbinu za kikatili katika kuwashughulikia wahalifu.
..the same kwa suala la Sumaye. je, amevunja sheria za matumizi ya mafao ya viongozi wastaafu? je, viongozi wastaafu hawaruhusiwi kuhudhuria mahubiri ya kidini wakiwa nje ya nchi? pia amehudhuria mahubiri mangapi, katika miji mingapi tofauti?
..ninachoomba mimi tuwe even handed. kama ni kupinga viongozi wakuu na wastaafu kutibiwa nje basi tusi-target wale tusiowapenda tu.
..hoja nyingine ya kanda2 ni kwamba Sumaye hana matatizo yoyote ya afya, na ushahidi wa hilo ni kwamba ameweza kusafiri "mikoani" Uk akitangaza dini. sasa ni viongozi wangapi wakuu wamewahi kufanyiwa check-up na baadaye wakaendelea na majukumu yao, safari na schedule nzito, kuliko alichofanya Sumaye?
..halafu angalia jinsi kanda2 anavyotumia neno "mikoani" akijaribu kujenga picha kwamba kusafiri ndani ya UK kunahitaji nguvu ya mtulinga sawa na kwenda Sumbawanga au Mingonyo.