Sumaye: Tusifurahie Bunge la chama kimoja

SERIKALI NDIO INATAKA BUNGE LA CHAMA KIMOJA NDIO MAANA ILIWATAFUTA WABUNGE FAKE 19 Kama DANGANYA TOTO kwa Wafadhili na ndio maana imekubali Kujitia HASARA YA Sh.Bil.8.2 kuwalipa MISHAHARA
 
Ndiyo maana anaitwa mr ziro.

Hajui kwamba wabunge hawajipeleki bungeni wanapelekwa na wananchi.

Huwezi kuwalazimisha wananchi wachague chama wasichokitaka.
2020 hapakuwa na uchaguzi kura zilipigwa siku 2 kabla ili marehemu apate 87% ccm mkwajuni watoto waliitwa na kupiga kura. Ushahidi upo
 
Sidhani kama kuna watu wengi na wa maana, wanaofurahia bunge la chama kimoja. Kwa hakika aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja ambaye wengi tunaamini hakuwa timamu. Naye huyo mwenyewe baada ya kufanya uharibifu wake aliofanya, dakika za mwisho kujua kuwa alichofanya ni usaliti mkubwa kwa taifa hili aliwehuka zaidi na kubuni ufumbuzi wa kosa lake kwa kosa lingine la wabunge wa upinzani kupitia viti maalum nje ya utaratibu uliowekwa. Watu wenye mapenzi mema, na zaidi hasa wazee wa nchi hii wanaofahamu nchi ilipotoka waache kutuimbia ngonjera zisizo na tija. Badala yake watutangulie katika hoja za msingi: mojawapo ni tafakuri ya kina ya nini kilitokea vyombo vyote vya nchi hii vikaacha kutumikia nchi na badala yake vyote vikamtumikia mtu mmoja? Na je, vyombo hivi havistahili kuwajibishwa?
 
Wajinga ndiyo waliwao. Faida ya multiparty ni kichukua dola ili utekeleze ilani ya Chama. Rais na mawaziri na wabunge na madiwani wanawajibika na hiyo Ilani, wasipotekeleza watatoka wote haijalishi huyu ni Mbunge au Waziri au IGP. Kelele za bungeni zilikuwapo 107 na zaidi kabla matusi ya tundulissu hayajawasambaratisha kabaki mmoja lakini mwisho wake ni kura siyo kelele. Samia ataanguka na kushuka, kupanda na kupeta, kwa jinsi Ilani inavyotekelezwa, siyo kw kumfukuza Boharia wa ATC. Kura 2025 zitaangali sera in totality, siyo nani aliiba ng'ombe. Dhana ya CHADEMA kwamba bunge liwe kari kw Rais wake au Waziri Bashe ni dhana potofu, haiwezekani. It will be handled internally.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…