ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mtu mmja ambae alikuwa ni Mkuu wa shule ya sekondari Chain bwana Peter Sewa amekutwa Amejinyonga Kwenye eneo la site alikokuwa anaendelea na ujenzi wa nyumba yake.
Polisi na familia wamethibitisha.
----
MKUU WA SHULE AJINYONGA HADI KUFA
Mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39 aliyetambulika kwa jina la Peter Mwile Sewa aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari ya chanji iliyopo katika kata ya chanji Halmashauri ya manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa amekutwa amejinyonga hadi kufa katika nyumba aliyokuwa akiijenga katika eneo la Utengule mkoani humo
Wakizungumza ndugu wa Marehemu pamoja na majirani wamesema Marehemu aliondoka nyumbani September 18 na kuelekea eneo lake la ujenzi ambapo baada ya muda mrefu kupita bila kuwa na mawasiliano na familia mke wa marehemu aliingiwa hofu na kuanza kutafuta marafiki zake ambapo waliamua kwenda katika eneo hilo na kukuta mwili huo.
Soma Pia: Mwalimu ajinyonga huko Moshi kisa riba kubwa ya mkopo
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa kaungwa John Mlumba Kubini amesema alipata taarifa hizo saanane usiku wa kuamkia leo, ambapo pamoja na mambo mengine ameitaka jamii kutokuchukua maamuzi ya haraka wanapo kuwa na matatizo na badala yake ni vyema kushirikisha watu wakaribu au viongozi ili kupata ufumbuzi.
--
My Take
Sio kawaida Kwa Walimu kuwa na stress ,hii imekuwa Mpya