Sumbawanga na ulaji wa kitoweo cha panya(wild rat)

GAS STATE

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,770
Reaction score
954
Asallam
nimeshtushwa na Habari toka mkoani Sumbawanga juu ya uwindaji na ulaji wa panya pori.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mkuu wa mkoa wa Sumbawanga ndugu Joachim Wangabo amemuagiza mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Khalfa Haule kuua panya kwa sumu ili kulinda misitu ambayo huchomwa moto na wananchi katika harakati za kuwinda panya. Ikumbukwe kuwa ili wawapate panya kwa urahisi wawindaji hao huchoma moto misitu then panya hukimbilia mashimoni na baadae huchimbwa na kuwapata bila usumbufu.


JOACHIM WANGABO RC SUMBAWANGA AKIONGEA NA WANANCHI


Panya wakiuzwa
Hoja yangu sio ulaji wa panya kwani ni msosi kama ilivyo mingine ila je ni asili yao au kwa sababu ya vyuma kukaza?
Kama ni asili kwa nini sio maarufu kama ilivyo mikoa mingine ambayo nayo kiumbe huyu ni fursa kwao.
WENYE UZOEFU NA SUMBAWANGA WATUJUZE ULAJI WA HAWA WADUDU MMEANZA LINI? JE SOKONI WANAPATIKANA?

Source: Global Publishers
 
Hii ni asili, ni mboga ya heshima kwa mfipa. Ila siyo hawa panya Wa ndani ni wale Wa porini.
 
Kuwa na heshima. Kitoweo cha wenzio we unaita wadudu.

Kiufupi panya ni kitoweo kitambo sana kwa maeneo hayo na siyo kwa sababu eti vyuma vimekaza ndio wameanza kula panya. Fuatilia historia
 
Wenzio wanaita yama wewe unaita wadudu...
Lkn nasikia wanakula panya buku
 
Usiniambie ati ata lile Pengo nalo lilikula au hata leo mnampelekeaga kwa hishima ya pengo lake. Dah!
 
Hii ni asili, ni mboga ya heshima kwa mfipa. Ila siyo hawa panya Wa ndani ni wale Wa porini.
Ok nikitaka kujuwa tu kumbe wala panya wako wengi nchini mbona mnawaandama makonde tu haahaaa
 
Daaa jamaa yangu mbona tunakwazana nimemiss sana hii kitu mnafosi nichukue likizo sasa
 
Hao Ni ndezi mjomba aka panya huku wanaliwa Na wanaprotini nyingi Sana.ni watam sana
 
Hao Ni ndezi mjomba aka panya huku wanaliwa Na wanaprotini nyingi Sana.ni watam sana
Safi sana mkuu kama wana virutubisho go on nilidhani tatizo vyuma kumbe ni local mxoxi
 
Awaaachie tu wapate kitoweo nyama ya ng'ombe imepanda bei
 
Ok nikitaka kujuwa tu kumbe wala panya wako wengi nchini mbona mnawaandama makonde tu haahaaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Rukwa/Katavi nako panya ni kitoweo cha heshima tu
 
Hakuna mkoa wa Sumbawanga mkuu, tuna mkoa wa Rukwa.. Wilaya ya sumbwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…