Sumu ni nini hasa ?

Sumu ni nini hasa ?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Waungwana wa JF,

Nawaomba wajuzi wanisaidie maana hasa ya sumu (poison) na aina yake.

Karibuni waungwana wa JF
 
Sumu ni kitu kinachoweza kusababisha kuumwa au kifo pale kinapoingia mwilini. Mara nyingi binadamu amekuwa makini na vitu anavyokula, kupaka mwilini, au kunywa ili asiingize sumu mwilini na kupata madhara. Pia sumu inaweza kuingia mwilini kwa kuvuta hewa, kuliwa, kupakwa au kugusa ngozi.

Aina nyingine ya sumu ni ile inayoingia katika akili. Kuna vitu unasikia, kusoma au kuona kisha vinakaa kwenye mind na kuathiri afya, hata kusababisha kifo.
 
Mkuu, Kuna namna yoyote ya kuondoa sumu iliyoingia katika 'akili' kabla haijaleta madhara makubwa?
 
Na mimi ninataka kuuliza, kwa nini ukila sumu ufe hua inaenda wapi hasa ndani ya mwili
Na kwa nini binaadamu akila asali hafi lakini mbuzi anakufa?
 
Mkuu, Kuna namna yoyote ya kuondoa sumu iliyoingia katika 'akili' kabla haijaleta madhara makubwa?

Ipo kabisa. Ni precedure ya kurudisha au kupunguza "sumu" katika akili na inachukua muda kutegemea ni aina gani ya athari na kiwango cha "sumu" hiyo. Therapists wengi wanafanya hii lakini kuna case tofauti na ujuzi tofauti.
 
Na mimi ninataka kuuliza, kwa nini ukila sumu ufe hua inaenda wapi hasa ndani ya mwili

Mkuu, kuna aina maelfu za sumu na reaction zake katika mwili zinatofautiana sana kutegemea na sumu yenyewe. Pia kuna sumu zinazoathiri haraka sana na zile za taratibu sana. Mfano wa sumu ya taratibu ni moshi wa sigara au tumbaku unaoathiri mapafu. Mara nyingi athari ni impairment na kama unavyojua baadhi ya organs zinategemeana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo fulani katika mwili unaweza kupelekea mifumo mingine ishindwe pia na mwisho kifo. Kwa uchache tu ni kwamba baadhi ya sumu husababisha kiumbe kushindwa kupumua, baadhi husababisha moyo kusimama baada ya sumu kuingilia mfumo wa misuli hivyo moyo kushindwa kuendelea kusukuma damu. Baadhi ya sumu humaliza nishati ya mwili kwa kuingilia mfumo wa seli na kuleta matokeo tofauti. hii inapokuwa katika seli nyingi na kwa kisai kikubwa basi ni mwanzo wa organs muhimu kama mapafu na moyo kusimama.

Na kwa nini binaadamu akila asali hafi lakini mbuzi anakufa?

Kuhusu hili la mbuzi kufa kwa kula asali sijui kwa hakika lakini kwa kuangali generally tu naweza kusema binadamu na mbuzi wametofautiana katika mifumo yao ya ulaji na uyeyushaji chakula. Wao ni herbivore wanakula mimea na vitu kama hivyo ili kuingiza carbohydrates kama nutrients katika miili yao. Sisi ni omnivores kwamba tunapata nutrients zetu either kwa kula wanyama au mimea. Kwa hiyo ingawa sijui ila nadhani katika tofauti hizi za digestion systems kunaweza kuwa utofauti mkubwa wa kuwafanya wao walapo asali iwe tatizo kwao (mbuzi). Katika matumbo yao wanakuwa na bacteria na vijidudu vingingi tofauti vinavyosaidia kuyeyusha majani kwa kuwa hayo ni tofauti na asali. Cellulose inayotokana na mimea haina nishati ya kutosha kama vijidudu na bacteria hawatasaidia kuiozesha na kuiyeyusha. Kuna uwezekano wa asali kugeuka sumu katika process ya digestion kwa herbivores digestion huchukua muda mrefu zaidi na vijidudu hivi huenda vikawa vinaathiriwa na asali ambayo ina sugar traits. Mtaalam wa wanyama anaweza kuwa specific zaidi au labda tofauti.
 
Sumu ni kitu kinachoweza kusababisha kuumwa au kifo pale kinapoingia mwilini. Mara nyingi binadamu amekuwa makini na vitu anavyokula, kupaka mwilini, au kunywa ili asiingize sumu mwilini na kupata madhara. Pia sumu inaweza kuingia mwilini kwa kuvuta hewa, kuliwa, kupakwa au kugusa ngozi.

Aina nyingine ya sumu ni ile inayoingia katika akili. Kuna vitu unasikia, kusoma au kuona kisha vinakaa kwenye mind na kuathiri afya, hata kusababisha kifo.

Naomba kujua uhusiano wa tango na asali ni vp vitu hivi ukila kwa pamoja hugeuka sumu?
 
Naomba kujua uhusiano wa tango na asali ni vp vitu hivi ukila kwa pamoja hugeuka sumu?

Mkuu, kuna baadhi ya vitu inategemea na mtu. Some wana allergies za aina mbalimbali na kunaweza kukawa na reaction mbaya kwa kuchanganya vyakula fulani. Nimeshawahi kuonja juice ya asali na tango na imechanganya na limao kidogo haina sumu au naweza kusema haikuwa na sumu kwangu. Kama uliwahi kupata shida kwa mchanganyiko huo then hiyo ni mbaya kwako na usijaribu bila kupata vipimo vya allergy.
 
Ipo kabisa. Ni precedure ya kurudisha au kupunguza "sumu" katika akili na inachukua muda kutegemea ni aina gani ya athari na kiwango cha "sumu" hiyo. Therapists wengi wanafanya hii lakini kuna case tofauti na ujuzi tofauti.

Shukrani Mkuu, swali la mwisho, Je, msongo wa mawazo unaweza kuzalisha sumu ya 'akili' yaani mfumo tu wa ubongo uka-generate hali inayoweza kugeuka sumu kichwani?
^^
 
Back
Top Bottom