Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Sumu ya chakula (Food poisoning) ni tatizo linalosababishwa na ulaji wa chakula kichafu kilichobeba vimelea vya magonjwa hasa bakteria na virusi, au sumu zake.
Vimelea hivi pamoja na sumu zake huathiri mfumo wa chakula kwenye sehemu za utumbo mkubwa na mdogo kisha kusababisha Maumivu makali ya tumbo, kuharisha, kutapika, kiungulia, uchovu na homa.
Dalili zake zinaweza kuanza kuonekana ndani ya dakika 30 au siku kadhaa baaada ya kutumia chakula husika.
Katika mazingira machache, tatizo la sumu ya chakula linaweza kuhatarisha afya kwa kusababisha upotevu wa maji mengi na chumvi muhimu za mwili, homa kali zaidi ya nyuzijoto 38.9, ugumu wa kuzungumza pamoja na kutoa choo chenye damu. Dalili hizi ni hatari kwa afya, zinaweza kumfanya mhusika apoteze uhai hivyo ni muhimu kupata msaada wa haraka hospitalini.
Jikinge na tatizo la Sumu ya Chakula (Food Poisoning) kwa kufanya mambo yafuatayo-

- Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kupika na kula vyakula.
- Tunza vyakula vyako sehemu safi na salama hasa ile isiyo ruhusu kuzaliana kwa vimelea vya magonjwa.
- Hakikisha unaivisha vizuri chakula chako pindi unapokuwa unapika ili kuangamiza sumu na vimelea vinavyoweza kusababisha tatizo hili.
- Safisha vizuri matunda na mboga za majani kabla ya kuvitumia.
- Chemsha chakula chako (kiporo) ili kipate joto la kutosha kabla ya kukitumia hasa ikiwa hakikutunzwa kwenye friji.