Doto Dotto
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 3,906
- 2,902
Aaah!! Jamaniii...!!!!Bashite kisha pigiwa parapanda inalia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaah!! Jamaniii...!!!!Bashite kisha pigiwa parapanda inalia
Part 2
Mwaka 1997 shushushu huyo alipandishwa cheo na kuingia Kurugenzi ya Uchambuzi na Ukandamizaji wa makundi ya uhalifu mkubwa, akiwa na wadhifa wa mtendaji mwandamizi na naibu mkuu wa Idara ya Saba.
Mwishoni mwa mwaka huo, shushushu huyo alitoa tuhuma nzito kuwa alipewa amri ya kumuua Boris.Mwaka uliofuata, Boris alimtambulisha Litvinenko kwa Vladmir Putin, rais wa sasa wa Russia lakini wakati huo akiwa shushushu mwandamizi wa FSB.
Tatizo ni kwamba Litvinenko alikuwa akipeleleza ufisadi ambao Putin anadaiwa kuwa mhusika. Mwaka huohuo, shushushu huyo na baadhi ya wenzake wallijitokeza hadharani kueleza kuhusu njama za kutaka kumuuwa tajiri Boris.Baada ya tukio hilo, shushushu huyo alitimuliwa FSB na Putin alitanabaisha kuwa ndiye aliyetoa uamuzi huo.
Oktoba 2000, Litvinenko alitoroka Russia na familia yake na kwend Uturuki ambako aliomba hifadhi ya ukimbizi katika Ubalozi wa Marekani jijini Ankara lakini maombi yake yalikataliwa. Inaaminika kuwa kukataliwa huko kulitokana na hofu kuwa kuyakubali maombi hayo kungezua matatizo kati ya Marekani na Russia. Mwaka huohuo,shushushu huyo alinunua tiketi ya kusafiri kwa ndege kutoka Ankara kwenda Moscow kupitia London, Uingereza. Alipofika uwanja wa ndege wa Heatrhow kusbiri ndege ya kwenda Moscow, shushushu huyo aliomba hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa, ambapo maombi yake yalikubaliwa mwaka mmoja baadaye, si kwa sababu ya uelewa wake wa mambo ya ushushushu bali kwa sababu za kibinaadamu (humanitarian grounds).
Wakati akiwa London, Litivnenko alijihusisha na uandishi wa habari, sambamba na kumsapoti tajiri Boris (aliyekimbilia Uingereza) katika mapambano ya kiharakati dhidi ya utawala wa Putin. Oktoba 2006, shushushu huyo alipatiwa uraia wa Uingereza.
Wakati huohuo, gazeti la Independent la Uingereza, liliripoti kuwa Litvinenko alikuwa akitumia na shirika la ujasusi la Uingereza, MI6 kutokana na ushahidi wa malipo yaliyokuwa yakifanywa na shirika hilo kwa shushushu huyo.
Mwaka 2007, gazeti moja la Poland lilidai kuwa picha ya Litvinenko ilikuwa ikitumika kwenye mazoezi ya kulenga shabaha (kama huelewi, hiyo ni ishara ya kuwindwa kuuawa). Kabla ya hapo, mwaka 2002, shushushu mmoja wa FSB, Mikhail Trepashkin, alimwonya Litvinenko kuwa kulikuwa na mpango wa kumuuwa uliokuwa ukiandaliwa na FSB. Mwaka huohuo, shushushu huyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za rushwa, japo alikuwa nje ya Russia.
Hata hivyo, wakati flani, wasifu wa shushushu huyo ulichafuka baada ya kupatikana taarifa kuwa alikuwa akiwatishia kuwaumbua matajiri kadhaa wa Russia kuhusu uhusika wao kwenye uhalifu mkubwa, na kudai pauni 10,000 kila mara ili asiwaumbue.
Wakati wa uhai wake, shushushu huyo alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya Putin, Russia na mwajiri wake wa zamani FSB. Miongoni mwa tuhuma hjizo ni Russia kuhusika na mashambulizi katika bunge la Armenia yaliyopelekea kifo cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Vazgen Sargsyan, FSB kufanya mauaji nchi Russia na kuwalaumu magaidi wa nje ili kupata uhalali wa kufanya ubabe nje ya nchi hiyo, mdai ya uhusiano kati ya Russia na Al-Qaeda, nk.
... .......Itaendelea
Wale wenye majina ya kiarabu mnaomuonaga Putin kama nabii oneni ushetani wakePart 1:
Ukisoma au kusikia balaa lililomwandama Alexander Litvinenko hadi kifo chake, waweza kudhani ni simulizi kutoka kwenye filamu au riwaya flani. Litvinenko alikuwa shushushu wa shirika la ushushushu la Russia, FSB, katika kitendo cha kubaliana na uhalifu mkubwa (organised crime). Kabla ya kuwa shushushu, Litvinenko alikuwa mwanajeshi ambapo alipanda cheo hadi kufikia ngazi ya ukamanda wa platuni.
Mwaka 1986, Litvinenko alianza kuingia kwenye taaluma ya ushushushu baada ya kuwa 'recruited' kuwa mtoa habari (informant) Shirika la zamani la ushushushu la Russia KGB, katika kitengo cha kupambana na ujasusi (counterintelligence). Miaka miwili baadaye, Litvinenko alihamishiwa rasmi KGB kwenye Kurugenzi Kuu ya Tatu iliyokuwa inahusika na military counterintelligence.
Mwaka huohuo, baada ya kuhudhuria mafunzo ya ushushushu, Litvinenko akawa shushushu kamili katika eneo la kupambana na ujasusi hadi mwaka 1991, ambapo alipandishwa cheo na kuingia katika Federal Counterintelligence Service, shirika la ushushushu baada ya KGB, ambalo lilidumu kutoka mwaka 1991 hadi 1995lilipoundwa upya kuwa shirika la sasa la ushushushu la Russia yaani FSB. Shushushu huyo alipangiwa kitengo kilichohusika na kukabiliana na ugaidi sambamba na kujipenyeza (infiltration) kwenye makundi ya uhalifu mkubwa.
Kadhalika, alikuwa na jukumu la kufuatilia 'maeneo ya moto' (hot spots), yaani maeneo nyeti ndani ya Russia na katika nchi znyingine zilizokuwa ndani ya USSR. Wakati wa vita ya Chechnya, Litvinenko alifanikiwa kupandikiza mashushushu kadhaa ndani ya Chechnya.
Mwaka 1994, Litvitenko alikutana na mmoja wa waliokuwa matajiri wakubwa nchini Russia, Boris Berezovsky alipokuwa anafuatilia jaribio la mauaji dhidi ya tajiri huyo.
Hatimaye akaanza kufanya kazi za pembeni kwa ajili ya Boris, na baadaye akawa msimamizi mkuu wa ulinzi wa kibopa huyo. Ofkoz 'ajira' hiyo ya Litvitenko kwa tajiri huyo ilikuwa sio halali lakini dola iliwavumilia hasa ikizingatiwa kuwa mishahara ya mashushushu kama yeye ilikuwa kiduchu.
Itaendelea
unaifahamu polonium 210 au unaisikiaga tu, ingekuwa yenye [/QUOTE]unaifahamu polonium 210 au unaisikiaga tu, ingekuwa yenye tusingekuwa naye.Poloniuma 210.
Mwaky-mango anaijua hii.
Putin ni mtu hatari hili Kila mtu anajua. Hata wafuasi wake wanajua. Hata wamagharibi wanajua!Wale wenye majina ya kiarabu mnaomuonaga Putin kama nabii oneni ushetani wake