Sungusungu wadaiwa kumpiga raia Shinyanga

Sungusungu wadaiwa kumpiga raia Shinyanga

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
azamtvtz-20230417-0002.jpg
azamtvtz-20230417-0001.jpg
azamtvtz-20230417-0003.jpg


SHINYANGA: Manka Mushi mwenye miaka 26 mkazi wa Ikoma, Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, amenusurika kifo baada ya kupigwa na Jeshi la Jadi Sungusungu kwa tuhuma za wizi wa Tsh 420,000.

Akizungumza na Azam News katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga alipolazwa akipatiwa matibabu, Manka amesema tukio hilo lilimsibu usiku wa Aprili 14, 2023 baada ya mwanaume aliyekuwa akimtaka kimapenzi kumkataa na kuamua kusema kuwa amemuibia pesa hizo.

Amesema baada ya tukio hilo, mwanaume huyo alimshika kwa nguvu na kumtishia kumuua kwa kumnyonga shingo hadi kupelekea kujisaidia haja kubwa ikatoka kisha kumfikisha kwa sungusungu ili aadhibiwe ambapo aliadhibiwa viboko vilivyochangia kupoteza fahamu.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Prisila Mushi amesema mtu huyo alipokelewa Aprili 14, 2023 akiwa na hali mbaya na baada ya matibabu anaendelea vema huku akiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili hususani makalio na mgongoni.

CHANZO: Azam TV
 
Back
Top Bottom